Habari za Punde

Anaswa naNoti Bandia za 3m/-

Na Charles Yohana,Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Ibrahimu Bakari (56) mkazi wa Lushoto mkoani Tanga, kwa kosa la kukutwa na noti bandia 304 za shilingi 10,000 kila moja ikiwa na namba tofauti, ambazo zote zina thamani ya shilingi milioni 3.04.

Kmanda wa polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 29 mwaka huu majira ya saa 14:15 mchana huko Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mtuhumiwa akijaribu kununua maji kwa kutumia noti mojawapo.

“Alitaka kununua maji kwa mfanyabiashara wa kituo cha mabasi akiwa kwenye basi alilokuwa akisafiria lakini bahati nzuri huyu muuza maji alishitushwa na noti hiyo ndipo alipotutaarifu na tulimfuatilia na baadae tukamkamata akiwa na kiasi hicho cha fedha bandia,” alisema.

Katika tukio jengine mkazi mmoja wa Rufiji mkoani humo, Hamis Omary (15) amekufa baada ya kung’atwa na mamba wakati alipokwenda kuteka maji kwenye mto Rufiji.

Alisema tukio hilo lilitokea Septemba 28 mwaka huu majira ya saa14:00 mchana na mwili wa marehemu ulipatikana Septemba29 ukiwa na majeraha kichwani na jeraha kubwa upande wa mkono wa kushoto huku ukiwa umenyofolewa mguu wa kushoto

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.