STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 29 Novemba, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za rambirambi Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu Philip Mangula kufuatia kifo cha mtoto wake Peter kilichotokea hivi karibuni.
Katika salamu hizo Dk. Shein amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mtoto wako mpenzi Peter kilichotokea tarehe 26 Novemba, 2013” na kuongeza kuwa kwa niaba yake, wanachama wa CCM Zanzibar wanatuma salamu za rambirambi kwake Ndugu Mangula, familia, jamaa na marafiki wote na wanaungana na wafiwa katika kuombleza msiba huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amekieleza kifo cha ndugu Peter kuwa ni pigo si kwa familia yake tu bali kwa Tanzania nzima kwa kuwa marehemu alikuwa mtu mwenye juhudi kubwa katika kazi na aliipenda nchi yake.
Dk. Shein amemuomba Mwenyezi Mungu ampe Ndugu Mangula na wafiwa wote subira na uvumilivu wakati huu wa kuomboleza msiba huo mkubwa.
No comments:
Post a Comment