MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mama Asha Balozi Seif na Mke wa Balozi Mdogo wa
China, Wu Yan, wakimsikiliza Amir Ali Khamis Mwinyi, akitowa maelezo ya
ujenzi wa madarasa ya skuli hiyo yanayojengwa na Uongozi wa Raudha Academy
Fuoni Ijitimai, wakiwa wa ziara ya kutembelea Skuli hiyo na kutowa misaada kwa watoto
yatima wanaoishi katika kituo hicho
Jengo la Skuli ya Raudha Acadamy Fuoni Ijitimai likiwa katika ujenzi wake likiwana madarasa manne.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitembelea ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Raudha Acadamy Fuoni Ijitimai, na kutoa msaada wa mifuko ya Saruji na Vitabu vya kusomea kwa Watoto Yatima wanaoishi katika kituo hicho na kupata elimu yao hapo.
WATOTO mayatima wanaoishi katika Kijiji cha
Markas Fuoni Ijitimai wakimsikiliza Mke
wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,
alipofika kuwakabidhi Vifaa vya skuli na mifuko ya cement kwa ajili ya ujenzi
wa madarasa ya kusomea
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serekali na Walezi na Walimu wa Skuli ya Raudha Acadamy Fuoni baada ya kutembelea Skuli hiyo na kutowa msaada kwa Watoto Yatimawanaoishi katika Kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment