Habari za Punde

Balozi Seif Akutana na Uongozi wa Zantel

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi, akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Mawasiliano kupitia mfumo wa satalaiti la Etisalat linaloendesha Kampuni ya Zantel Bwana Pralap Ghose, alipofika Ofisini kwake Vuga leo kwa shughuli za kikazi.
Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Zantel Zanzibar Mohamed Mussa { aliyevaa Miwani } na Mwenzake kulia Meneja wa Mahusiano ya Serikali Ofisi ya Dar es salaam Charles Jutta wakifuatilia mazungomzo ya Balozi Seif na Mwakilishi wa Shirika la Etisalat Bwana Pralap Ghose hawapo pichani.
Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Zantel Zanzibar Mohamed Mussa na kulia Meneja wa Mahusiano wa Zantel Ofisi ya Dar es salaam Charles Jutta wakifuatilia mazungomzo ya Balozi Seif na Mwakilishi wa Shirika la Etisalat Bwana Pralap Ghose hawapo pichani.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza Bwana Pralap Ghose kufuatia shirika lake la Kimataifa la Etisalat linaloendesha Kampuni ya Zantel jinsi linavyotoa huduma bora za mawasiliano kupitia simu za mikononi pamoja na mitandao ya internet.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR).

1 comment:

  1. Kama sikosei nafkiri jina la huyo CEO ni Pratap Ghose na si Pralap kama ilivoandikwa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.