Duniani kila mtu ana starehe zake na jinsi ya kupoteza time kwa kuangalia njiwa wake kama mdau huyu akiwa katika mitaa ya michezani akipozi kwa kuangalia mifugo yake..
Mdau huyu akiwa na njiwa wake akiwapa chakula na kupoteza mawazo wakati wa jioni akiwa na ndege wake aina ya njiwa.Vijana wengi katika Visiwa vya Unguja hupenda kufuga njiwa na ndege wa aina mbalimbali. Katika kipindi hichi njiwa huwa na bei kubwa kwa seti moja huuzwa mpaka shilingi laki moja kutokana na kabila yake .
Kuna njiwa aina ya Manga, Shore Masoksi na kadhalika.
Unanikumbusha mbali huku mashozi akinimwagika nikiwa kijana mdogo katika mitaa ya Gulioni nafuga njia enzi hizo Rais wetu alikuwa Mzee Aboud Jumbe Mwinyi Mmungu ampe afya na nguvu nilikuwa nafuga nyiwa aina ya Hudhurungi na chafu chafu wakaja vijana kutoka mtaa wa muembe Makumbi miongoni mwao alikuwa kijana mmoja itwae Masoud au seif kama sikosei akaniibia njiwa wangu bada zima walikuwa wengi nilipatwa na machungu n kilio sana mpka leo sijamsamehe sio hapa tu hadi mbele ya Mmungu itakapotolewa hukumu kwani njiwa wale niliwanunuwa kwa tabu sana kutokana na pesa jinsi nilivyokuwa nazipata ,tulikuwa tunalima mchicha pale mlandege mbele ya wagonga vyuma nilikuwa na sehemu yangu ya kupanda mboga mboga na kutilia maji kila jioni pesa nizipatazo kwa kuuza mchicha huwa nanunuwa njiwa wale hudhurungi na chafu chafu walikuwa ndio wenye hadhi
ReplyDelete