Habari za Punde

JK aagiza maghala ya chakula yafunguliwe kusaidia waathirika wa mafuriko

Na Farida Msengwa,Magole
RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza bohari ya chakula nchini kufungua maghala yake ili chakuka likichomo kipelekwe kwa watu walioathiriwa na mafuriko katika tarafa ya Magole mkoani Morogoro.
Pia aliamuagiza Waziri anayeshughuliki maafa, Willium Lukuvi, kuhakikisha waathirika wa mafuriko wanasaidiwa haraka ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba.
Akizungumza na waathirika wa mafuriko katika skuli ya sekondari Magole baada ya kukagua athari za mafuriko, Rais Kikwete alisema mbali na waathirika kupata baadhi ya misaada, serikali itafungua maghala yake na kuwasambazia chakula.
“Hili la chakula na makazi ondoeni shaka,kwanza tunakwenda kufungua ghala letu la taifa na kama kutakuwa na upungufu wa aina yoyote ya chakula serikali itanunua kujazia, kuhusu makazi naliagiza Jeshi la Wanachi kuanza kazi hii mapema  maana tukiwapa kazi hii halmashauri watu wataishia kujenga nyumba zao tu,” alisema.
Akionyesha imani ya utendaji bora na nidhamu katika matumizi ya fedha za umma,  alisema kwa kuanzia zitajengwa zaidi ya nyumba 200 za mabati juu na chini na kuwagawia.
Akionyesha kutofurahishwa kwa mpango wa dharula wa kuwaweka wanaume mbali na wanawame pasipokujali nasaba zao, aliwataka Wakuu wa mikoa iliyokumbwa na mafuriko,Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wao kufanya tathimini ya kina juu ya waathirika na malizao ili serikali iweze kuwasaidia.

Aidha ameviagiza viwanda vya magodoro nchini kupeleka magodoro kwa waathirika hao ili waepukane na kulala chini kwenye unyevunyevu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.