Habari za Punde

Mchezo wa Ufunguzi Kombe la Mapinduzi Simba na Leopard.Simba Inaongoza kwa Bao moja.


Kocha wa timu ya Taifa ya Italia akiwapungua mikono Mashabiki wa Mchezo wa Mpira katika mchezo wa Ufunguzi uliozikutanisha timu za Simba na Leopard.
                    Vikosi vya timu za Simba na Leopard vikingia uwanjani kwa mpambano wao
                  Kikosi cha timu ya Leopard kilichocheza na Simba usiku huu na kukubali kufungwa bao moja
Kikosi cha timu ya Simba kilichoizamisha timu ya Leopard ya Kenya katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi usiku huu.
Viongozi wa Jukwaa Kuu wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa kombe la Mapinduzi uliofanyika katika uwanja wa amaan usiku huu,ulozikutanisha timu za Simba ya Tanzania na timu ya Leopard ya Kenya, katika mchezo huu timu ya Simba imeshinda bao 1--0, kupitia mchezaji wake Amiri Kiemba katika kipindi cha pili cha mchezo huo. 
Mchezaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Leopard, wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi
Nimepita ndivyo inavyoonekana mchezaji huyu wa timu ya Simba akimramba chenga beki wa timu ya Leopard.
              Mchezaji wa timu ya Simba akizuia mpira huku beki wa timu ya Leopard akijaribu kumzuiya.
                                                        Hapa tayari nimeshapita wacha wewe
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao baada ya kuandika bao la kwanza katika kipindi cha pili cha mchezo huo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi mchezo unaofanyika usiku huu katika uwanja wa Amaan. Simba imeshinda 1--0

Washabiki wa mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Leopard, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.Timu ya Simba imeshinda mchezo huo. kwa bao 1-0 
 Wachezaji wa timu ya KCC ya Uganda wakifuatilia mchezo huo wa timu ya Leopard na Simba, uliofanyika usiku, Timu ya KCC imecheza jiona na timu ya KMKM , na kuibuka na ushinda wa mabao 3--1
 Mchezaji wa timu ya Simba akiokoa mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Leopard
 Washabiki wa mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Leopard, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.Timu ya Simba imeshinda mchezo huo. kwa bao 1-0
 Wachezaji wa timu ya Simba  wakifuatilia mchezo huo.
Mshambuliaji wa timu ya Leopard akijaribu kumpita beki wa timu ya Simba katika mchezo wa ufunguzi wa Mapinduzi Cup, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaan usiku huu. Timu ya Simba imeshinda kwa bao 1--0

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.