Habari za Punde

Mgombea wa CCM Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Suluhu Ali Rashid, akitowa maelezo kwa mgombea wa CCM alipofika kuchukua fomu ya kugombea Uwakilishi katika Ofisi za Tume Maisara. 
MGOMBEA nafasi ya Uwakilishi katika Uchaguzi mdogo wa  Jimbo la Kiembesamaki Bwa,Mahmoud Thabit Kombo, akikabidhiwa Fomu ya kugombea nafasi hiyo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Suluhu Ali Rashid, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara

                       Akionesha fomu zake baada ya kukabidhiwa na Afisi wa Tume ya Uchaguzi




Mgombea wa Uwakilishi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki Bwa Mahmoud Thabit Kombo akionesha Fomu zake za kugombea nafasi hiyo ya Uwakilishi ya Jimbo la Kiembesamaki baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Mahmoud Thibit Kombo akishindikizwa na Wanachama wa CCM wa jimbo la Kiembesamaki baada ya kuchukuwa Fomu za kugombea Uwakilishi kupitia uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mwazoni mwa mwezi wa Febeary 2014, kuziba nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid aliyevuliwa Uwanachama wa CCM na Chama chake mwaka jana.
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Bwa Nahamoud Thabit Kombo akiondoka katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi kwa kushindikizwa na wapanda Pikipiki kuelekea katika Ofisi za CCM tawi la Kiembesamaki kwa mazungumzo na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Kiembesamaki. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.