Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis.
Habari za mchana ndugu wanahabari,
tumewaita ili kutoa taarifa kwa wananchi
juu ya tukio ambalo limetokea ndani ya Mkoa wetu ambalo kwa kiasi kikubwa
linataka ufafanuzi kutokana na jinsi linavyozungumzwa huko nje.
Siku ya tarehe 13/01/2014 majira saa
9:55 jioni hapo Rahaleo kwa Mchina Tambi palitokea tukio la unyangani wa
kutumia silaha. Tukio hili lilitokea wakati
Bw: SAID SEIF SALAMI 34, Riami
wa RAHALEO ambaye ni MFANYA BIASHARA wa vyakula anayefanyia biashara yake
Kibanda Maiti na anaishi mtaa wa RAHALEO alipofanyiwa unyanganyi huo.
Mfanya biashara huyu alifunga biashara
yake majira ya saa 9:45 jioni ya siku hiyo ya tarehe 13/01/2014 na kuchukua
pesa za mauzo ya kutwa jumla ya T.sh 11,500,000/= ambazo alizifunga katika
bahasha /mfuko wa kaki na kuondoka nazo kuelekea nyumbani kwa kutumia gari yake
no. Z. 128 EW NISSAN Rangi ya silver. Alipofika maeneo ya Raha Leo Kwa Mchina
Tambi ndipo gari moja yenye no. Z.866 EX aina ya SCUDO ilipomzinga kwa
mbele na ghafla aliona watu watatu wametokezea wakiwa na silaha mbili, moja
ikiwa ni bastola na nyengine ni SMG. Watu hao walimlazimisha kwa usalama wake
awape ule mfuko wenye pesa. Kwa kuhofia usalama wake alitoa pesa zote jumla ya
T.SH 11,500,000/=
Majambazi hao baada ya kitendo hicho cha
kuchukua hizo pesa walikimbilia kwenye gari yao. Kitendo hicho kilifanyika
mbele ya watu ambao walianza kupiga kelele za mwizi!, mwizi!, mwizi!, kelele
ambazo zilimfanya dereva wa gari ya majambazi kuondosha gari na kuwaacha wenzao
watatu chini.
Wakati huo wananchi walipiga simu Polisi
huku juhudi za ukamataji zikiendelea.
Polisi walifika eneo la tukio na kumkuta
mtuhumiwa mmoja asiye na silaha akiwa tayari amekamatwa kwa msaada wa wananchi.
Mtuhumiwa huyo anaitwa MAULID ALI @ KIPARA. Juhudi ziliendelea kufanywa
kuwafuatilia majambazi wengine walioondoka
eneo la tukio na silaha. Miongoni mwao jambazi mmoja alifanikiwa kuitupa
silaha aina ya SMG isiyo na magazine na shuka la kimasai ambalo alikuwa amevaa
Jambazi huyo kujaribu kubadilisha utambulisho wake. Silaha na shuka hilo la
kimasai vilitupwa hapo eneo la ndani ya msikiti wa Muembe Shauri. Jambazi huyu
aliruka ukuta na kutokomea upande wa pili.
Mtuhumiwa wa tatu aliyekuwa na pistol
alikabiliwa na Wananchi wa maeneo ya Kwa Ali Natoo kwa kushirikiana na Askari
wetu wa vyombo mbalimbali wakiwemo Polisi, KMKM, JKU na Mafunzo na walifanikiwa
kumkamata akiwa na hiyo Pistol aina GLOG 17 ikiwa na no. PPG 617 ikiwa na risasi zake17
ambayo alikamatwa nayo Mtuhumiwa huyo aitwaye GANGIRA CHARLES MSHANDETE 34,
MSUKUMA WA DSM anayesadikiwa kuwa ni
mtumishi wa PCCB DSM kutokana na maelezo yake lakini pia kitambulisho na silaha
yake vinaonyesha kumilikiwa na Taasisi hiyo.
Baada ya mahojiano kuanza, mtuhumiwa wa
kwanza alitowa ushirikiano wa namna ya kumpata mshirika wao ambaye aliendesha
gari la Majambazi, hivyo Mtuhumiwa huyo dereva alikamatwa maneo ya Shangani
nyuma ya African House nyakati za Magharibi. Mtuhumiwa huyo wa tatu anaitwa KHAMIS
FAKI HAJI 40, MSHIRAZI WA MWERA. Baadaye Mtuhumiwa huyo alitoa ushirikiano
wa kuitoa gari iliyofanyia tukio ambayo tayari alikuwa ameshaificha ndani ya
eneo la viwanda vidogo vidogo. Gari hiyo ina no. Z 866 EX aina ya SUZUKI ambayo
ndiyo iliyotumika katika ujambazi.
Baada ya kukamatwa dereva huyo,
mtuhumiwa wa kwanza aliendelea kutoa ushirikiano kwa kumvuta mtuhumiwa
aliyeitupa Bunduki ya SMG pale msikitini Muembe Shauri. Ilipendekezwa itumike
gari ya mtuhumiwa wa tatu ili kumfanya yule anayevutwa asishituke. Wapelelezi
na Mtuhumiwa wa kwanza walienda hadi eneo walilokubaliana kukutana. Walipofika
pale na ishara ilitolewa ili afike, lakini
wakati unafunguliwa mlango wa gari alibaini kuwa waliokuwemo ni Askari
na hivyo alitimka mbio. Juhudi zilifanyika na akakamatwa. Mtuhumiwa huyo wanne
anajulikana kwa jina la RAJAB MOHAMED BAKAR 25, MSHIRAZI WA KOROGWE TANGA. Licha
ya mtuhumiwa huyu kujitambulisha kwa jina hilo wenzake wanamtambua kwa jina la CHRISTOPHER
MKAAZI WA KIGOMA – MUHA. Mtuhumiwa huyu alipopekuliwa alipatikana na silaha
nyingine ya Pistol aina ya Browning yenye namba TZ CAR 93480. Hizi ni namba
mpya za silaha ambazo kupitia data base ya CAR DSM tunaweza kujuwa mmiliki
halali wa silaha hii na jinsi gani imetoka mikononi mwake pengine inawezekan na
yeye akawa ni mshiriki wa kosa la ujambazi. Pia pistol hiyo ilikuwa na risasi
moja.
Kwa ufupi katika tukio hili silaha
zilizokamatwa ni tatu ikiwemo SMG moja na pistol mbili na risasi 18 jumla.
Kuhusu mali zilizoibiwa pesa taslim T.sh
3,900,000/= zimepatikana na kwamba mtuhumiwa wa pili ndiye aliyekamatwa nazo
pamoja na simu ya mlalamikaji, kadi ya Benki na leseni ya udereva. Katika
sakata la ukamataji Mtuhumiwa huyu aliutupa ule mfuko wa pesa na mtoto mmoja
aliuchukua na kukimbia nao. Juhudi zilifanywa na akapatikana akiwa
ameshawakabidhi kaka zake ambao walirejesha jumla ya T.sh 3,900,000/= huku
mfuko uliokuwa umehifadhi ukiwa umechanwa hali ya kuwa awali walipokabidhiwa na
huyo mtoto mfuko huo ulikuwa umefungwa vizuri. Mtu mmoja anashikiliwa kuwezesha
upatikanaji wa mali zilizobakia. Kwa jumla walikamatwa watu saba na kuhojiwa
katika tukio zima.
Sambamba na taarifa hiyo napenda pia
kuwaonyesha bunduki aina ya Gobore tuliyoikamata tarehe 03/01/2014 saa 1:00
usiku huko Fuoni Mkoa wa Kusini Unguja
pamoja na watuhumiwa watatu ambao walikuwa wanajiandaa kufanya ujambazi kwa
BAKHRESA Mtoni Unguja walikamatwa wakiwa na silaha hiyo ya Gobore yenye kutumia
risasi za Shortgun
Watuhumiwa hao ni 1. ISMAIL HAJI SADI @
GREY, MSUKUMA WA AMANI KWA MABATA
2. ALI MOHAMED ALI@ BAB ALLY, FUNDI ALI,
WA FUONI
3. OMAR ISSA MOHAMED, MSHIRAZI WA DSM
Watuhumiwa hawa leo tarehe 16/01/2014
tumawapeleka Mahakamani.
Naomba kutumia nafasi hii kwa mara
nyengine tena kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wote kwa ushirikiano wao
katika mapambano na majambazi tuliofanikiwa kuwakamata tarehe 13/01/2014.
Tunawaomba wananchi kutoa ushirikiano
kwa Jeshi lao la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazoweza kusaidia kuwakamata
wahusika wa matukio kama haya ambao
lengo lao ni kujipatia mali kwa njia ya mkato lakini pia kuleta hofu na
taharuki kwa wananchi.
Nawashukuru, Asanteni sana.
.
Hongera kwa wananchi na jeshi la polisi, kwa pamoja tunaweza.
ReplyDeleteAfadhali Mussa ameenda sasa kazi inafanyika! Mussa kazi yake ilikua ni porojo na uchochezi!
ReplyDeleteAliwahi kuzungumza na waandishi wa khabari na kusema eti Z'bar kuna magaidi na kusababisha kuporomoka kwa biashara ya utalii! alisahau kua hata hizo nchi zenye MAGAIDI kama KENYA hua hazitaki kukiri zenyewe!
Hongera jeshi la Polisi!
hii ni fix ya kipolisi yenye madhumuni ya kunufaisha wanasiasa wenye kutaka muungano , kwa sababu sisi waznz huwa tunalalamika ujambazi huwa unafanywa na watu wa tanganyika , kwa hio wakaipanga hii fix na kutuonyesha majina ya watu hao kama ni wazanzibari , acheni mambo ya upuuzi , ujambazi wa znz bado unafanywa na watanganyika hata mkijaribu kufanya nini , hizi triki za kitoto zimepitwa na wakati , kuweni watu wazima
ReplyDeleteHivi ndivyo polisi wanatakiwa wafanye sio kupiga watu kwenye mikutano. Hongera kamishna mpya kwa juhudi yako unayoionesha sio kama yule aliokuwa akitumia mbinu mpya za kukamata watu wasio na hatia
ReplyDeletehii ni aibu kwa chombo cha usalama kama TAKUKURU
ReplyDelete