Na kadama Malunde, Shinyanga
ASILIMIA 70 ya Watanzania wanaohukumiwa vifungo
magerezani, wanafungwa kwa sababu ya kutojua sheria na kutopata msaada wa
kisheria.
Hali hiyo imebainishwa mwishoni mwa wiki
iliyopita wakati wa mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo viongozi wa asasi
zinazojishughulisha na utoaji wa huduma za kisheria mkoani Shinyanga
yaliyoendeshwa na Mtandao wa watoa huduma wa msaada wa kisheria nchini
(TANLAP).
Mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo,Edna Bakebwa,
ambaye ni mwanasheria wa kutoka TANLAP, alisema utafiti uliofanywa hivi
karibuni umebaini asilimia 70 ya watu waliomo magerezani walitiwa hatiani
kutokana na kutozijua vyema sheria za nchi.
Alisema kutokana na kutojua haki huwafanya
kushindwa kujitetea vizuri na hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuielimisha
jamii kujua haki zao.
Alisema watoa huduma za kisheria wana fursa ya
kuwatembelea wafungwa waliomo magerezani na kuelimishwa juu ya haki zao za
msingi kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwamba kwa wale wanaofikishwa katika
vituo vya polisi wanayo haki ya kutoa maelezo yao mbele ya mtu au wakili wanayemtaka.
Katika hatua nyingine alisema si tabia nzuri ya
watoa huduma za msaada wa kisheria kukaa bila ya kuielimisha jamii juu ya haki
zao za msingi na kusubiri mpaka pale wanapopatwa na matatizo ndipo hujitokeza
kwenda mahakamani kuwapatia msaada wa kisheria.
“Katika utafiti uliofanywa mwaka 2011/2012
tulibaini asilimia 70 ya watu waliomo magerezani walifungwa kutokana na
kutozijua sheria za nchi na hata haki zao za msingi kwa mujibu wa katiba, sasa
hili ni tatizo ambalo nyinyi kama watoa huduma za msaada wa kisheria mnapaswa
kulifanyia kazi,” alisema.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamewaomba wajumbe
wa bunge maalumu la katiba kuhakikisha
wanajadili rasimu ya pili bila ya kutanguliza maslahi ya vyama vyao
No comments:
Post a Comment