Na Kunze Mswanyama, DSM
NAIBU Waziri wa zamani wa Mifugo na Maendeleo ya
Uvuvi,Dk.James Wanyancha,amewataka wabunge wa bunge maalum la katiba,
kuhakikisha wanatetea maslahi ya umma na kuacha kulumbana juu ya maslahi ya
vyama au taasisi zilizowachagua.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Dk.Wanyancha, alisema kwa sasa taifa liko njia
panda kutokana na mapendekezo ya serikali moja,mbili na wengine wakitaka
serikali tatu jambo ambalo anahisi ndiyo litaleta shida kwenye bunge hilo .
“Nawaomba wabunge hawa wasijadili kwa siasa, watatuletea
shida kubwa baadae kwani tume ziliundwa nyingi zote zilitaka serikali tatu,tume
ya Robert Kisanga na Francis Nyalali zote zilielekeza huko laikini ilipingwa sana , sasa mambo
yamegeuka na hatimae naamini itapita,” alisema.
“Wakati wa serikali tatu umefika nawaomba wabunge
wote wakubaliane na matakwa ya wananchi kwa kuwa hayo ni mawazo yao, katiba ni
mali ya Watanzania wote siyo ya baadhi tu, hivyo nawaomba wasichakachue mawazo
ya Watanzania,” alisema.
Akizungumzia kuhusu vita dhidi ya ujangili,Mbunge
huyo wa zamani wa jimbo la Serengeti, alimuomba rais Kikwete awataje mapapa 40
wa ujangili aliosema anawatambua ili kuhakikisha vita hiyo vinapiganwa
hadharani lakini kwa mafanikio makubwa.
Akiwa Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita,Rais
Kikwete aliiambia dunia kupitia mkutano ulioandaliwa na motto wa Malikia wa
Uingereza na kuhusisha nchi zaidi na 30
na mashirika 13 ya kimataifa kuwa,tayari serikali imebaini mtandao mpana wa majAngili
hao na kwamba jitihada zinafanyika kuuzima kabisa.
“Sidhani kama rais anaogopa kuwataja kwa kuwa
yeye analindwa na sheria, awataje ili tuwajue wahujumu wa rasilimali zetu, tunahangaika
kupiga kelele za majngili, oparesheni nyingi kumbe rais anawajua majangili hao
lakini hataki kuwataja, naomba awaambie Watanzania ili walinde rasilimali zao
kwa nguvu zote,” alisema.
Alisema kama serikali haitakuwa radhi kupambana
na majngil, vita hivyo havitakwisha.
Kuhusu wafanyakazi ambao wanatakiwa kustaafu, aliwataka
kujiandaa mapema kwani hakuna namna itakayomfanya mfanyakazi asistaafu utumishi
wake.
Alisema kustaafu siyo tiketi ya kifo kwani
watumishi wengi hudhani akishastaafu tu ndiyo itakuwa mwisho wake wa kuishi
duniani.
Kuhusu siasa, alisema anatarajia kuutarifu umma
kuhusiana na matarajio yake ya baadae kisiasa ambapo muda ukifika atajua kama arudi kwenye siasa au la.
No comments:
Post a Comment