Na Zainab Atupae, PEMBA
TIMU ya Machomane imeanza vyema mzunguko wake wa
pili, kwa kuichapa timu ya Young Eleven kwa magoli, 3-2 kwenye mchezo wa ligi daraja la pili
taifa Pemba uliochezwa.
Katika
ngarambe hiyo ambayo awali ilishindwa kutabirika ni nani engeibuka nas ushindi,
timu ya Machomane, ndio iliokuwa ya mwanzo kujipatia goli la kwanza kupitia
mchezaji Nassri Juma dakika ya 36.
Goli
lapili liliwekwa wwavuni na Ali Said dakika ya 72, huku goli la tatu na la ushindi
kwa Machomane, lilifungwa na Ghalbu Abeid
dakika ya 87, huku magoli ya
Young Eleven, yalifungwa na Abdllah
Mohamed dakika ya 61 na goli la
pili lilipachikwa na mcheza Mbarouk Ali
dakika ya 82.
Kwa
matokeo hayo timu Machomanne imefikisha alama 22 na kushika nafasi ya nne, na
kuwaacha Young eleven na alama zao 11.
No comments:
Post a Comment