Na.Salum Simba, MUM
NAWAPONGEZA
wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha pili waliofanya vizuri mitihani yao
lakini sijawasahau wanafunzi waliofeli wasivunjike moyo kwani kufeli kimasomo
si kufeli kimaisha.
Waliofeli
wanayo nafasi ya kujiendeleza kimasomo na hatimaye kufanya vizuri masomo
yao.
Wanafunzi
waliopasi katika mitihani yao iliyotangazwa hivi karibuni na waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali kwenye mkutano na waandishi wa habari inaonesha wazi
kiwango kimepanda.
Nafikiri
wanafunzi wanapaswa kusahau matokeo walioyapata wafanye juhudi ya kutosha ili
kupata matokeo mazuri huko wanakokwenda, kwani tumesahau matokeo ya mwaka jana
ya kidato cha nne zaidi ya asilimia 57 ya wanafunzi Tanzania walipata daraja
ziro na kuhesabiwa hata aliyepata pasi mbili yaani “D” amefaulu hali ya kuwa
hawezi kwenda popote kwa cheti chake.
Hapa
tunapata funzo tusichekelee kwa kufaulu lakini tutathimini mitihani mingine
kwani waswahili husema safari moja huanzisha nyengine, kwa hali hiyo juhudi
zahitajika kwa kukamilisha safari hiyo.
Wanafunzi
wengi hutumia nafasi walizozipata kulewa sifa za kupongezwa kwa kupasi kwao
vizuri na kusahau wajibu wao wa kusoma kwa bidii. Aidha wanasahau kuwa ‘elimu
ni ufunguo wa maisha’, ‘elimu ni nuru’.
Wengine
utawasikia wakijisemea shida yangu ilikuwa kuvaa “black and white” hata
nikifeli mtihani wa kidato cha nne nishazivaa na mimi nimetangazwa kwenye Radio
ama wengine wanasema mtihani wa kidato cha nne na cha sita ni ya Tanzania bara
hata nikijitahidi vipi nitafelishwa tu.
Nafikiri
matokeo mabaya ya kidato cha nne na cha sita yalitokana na kutochukua
bidii katika masomo. Mbali na kuwepo sababu nyengine kadhaa zinazochangiwa na
mazingira ya masomo lakini ifahamike hivyo
Wanafunzi
ya wamekuwa wakitamani maisha anasa kama vile kumiliki simu za kisasa, nguo
nzuri na mengine mengi, pia baadhi ya wanafunzi wanajihusisha na masuala ya
mapenzi mapema jambo linalowaingiza katika maisha hatarishi na yasiyo salama ya
kupata ujauzito na kupoteza haki yao ya masomo.
Matumizi
mabaya ya mitandoa ya kijamii kama vile facebook, viber, twiter na what
is up (wasap) imewapotezea muda wao mwingi ambao ungewafaa katika
kudurusu masomo yao.
Ifahamike
kuwa zaidi ya wanafunzi 80,000 wa chuo kikuu huhitimu kila mwaka, je wewe
mwenzangu na mimi uliyrridhika na matokeo ya kidato cha pili na darasa la saba
itakuaje katika soko la ajira?
Nina
wasiwasi nikiyakumbuka matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana, kama wanafunzi
wa Zanzibar hawatokuwa makini kwa kujiandaa kiume ili kukabiliana na mtihani
hiyo tutakuwa tukipasisha wanafunzi wengi darasa la saba na kidato cha pili
lakini tutakuwa tunafeli wengi kidato cha nne na cha sita kwa kulewa na
kuridhika kwa matokeo tuliyoyapata hapo awali.
Wanafunzi
wanapaswa kubadilika kwa kuyavua majoho ya sifa walizopewa na kupongezwa
mitaani kwa kufanya vizuri lakini waliowapongeza watawasubiri tena kwa matokeo
mengine.
Walimu
nao wanapaswa kufundisha kwa kadri wawezavyo na wahisi wanafunzi
wanaowafundisha ni sawa na watoto wao au ndugu badala ya kuwapa maneno ya
kuvunja moyo.
Baadhi
ya walimu wamekosa uvumilivu, ubunifu busara na hekma katika ufundishaji
hali ambayo inapelekea wanafunzi kufanya vibaya masomo yao kwasababu walimu
wengi kushindwa kutumia taaluma za kisaikolojia walizozipata wakati wanajifunza
fani ya ualimu.
Natambua
wazi na wala hakuna kificho kuwa walimu ni mihimili bora kwa maisha yetu kwani
hata mimi binafsi nisingeweza kupata taaluma hii kama kusingekuwa na juhudi za
walimu kutumika kwa kunifundisha kwao misingi bora ya kisoma kwa bidii.
Ipo
haja kwa kila mmoja kuchukua juhudi kuimarisha elimu ili kuleta matokeo
yaliyo bora kwa wanafunzi.

No comments:
Post a Comment