Na
Mwandishi wetu
KAMATI
ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara ya kutembelea barabara zinazotarajiwa
kuanza kujengwa pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kupunguza
msongamano.
Kamati
hiyo ambayo ilifanya mazungumzo na Waziri wa Ujenzi na watendaji wa wizara, ilikuwa ilikagua miradi
inayotekelezwa na wakala wa barabara Tanzania (Tanroads) katika mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza
na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Dk. John Magufuli, alisema mbali na utekelezaji wa miradi mbali mbali
mikubwa ya maendeleo jijini Dar es Salaam, pia upo mradi maalum wa kupunguza
msongamano kwa kuimarisha barabara zilizoko pembezoni mwa jiji ambazo ni viungo
muhimu kwa barabara kuu zinazoingia na kutoka mjini.
Alisema
katika awamu ya kwanza tayari jumla ya kilometa 22 kati ya kilometa 78.9 za
barabara hizo zimejengwa.
Barabara
hizo ni kuanzia kituo cha mabasi Ubungo kupitia Kigogo hadi barabara ya Kawawa
(km 6.4) na kutoka makutano ya barabara ya Kigogo kupitia bonde la Msimbazi
hadi makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga (km 2.72).
Alisema
barabara nyingine ni Jet Corner–Vituka– Devis Corner (km 12) na Ubungo Maziwa-Mabibo
External Mandela yenye urefu wa kilimota 0.64.
Alisema
katika mwaka huu wa fedha 2013/2014 jumla ya kilometa 27.2 zitaanza kujengwa
ikiwa ni awamu ya pili ya mpango huo.
No comments:
Post a Comment