Na Pascal Buyaga,MUSOMA
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA), Dk.
Wilbroad Slaa amesisitiza kwamba kama
chama hicho kitashika hatamu za dola, kitahalalisha pombe ya kienyeji aina ya
gongo.
Alirejea kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
viwanja vya Mukendo manispaa ya Musoma katika operesheni ya M4C pamoja daima.
Alisema wananchi wamekuwa wakikamatwa kwa kupika pombe aina ya gongo
na kuitwa haramu licha ya kuwaingizia
kipato wananchi, hivyo CHADEMA inakusudia kuiboresha pombe hiyo kwa
kuagiza mitambo ya kisasa.
“Wasomi,mawaziri na kada nyengine mbalimbali wengi wetu tumesomeshwa
kwa fedha za gongo, mama zetu na baba zetu wamekuwa wakipika kwa kificho, kwa nini tuendelee kuiita haramu,” alihoji.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamesema kauli hiyo inaashiria jinsi
CHADEMA kinavyojaribu kuchochea unywaji pombe na kudhoofisha nguvu kazi za
vijana.
Sasa imeanza kueleweka wazi kwa matamshi kama hayo,Chadema sasa imefilisika kisera. Chadema msitegemee kushinda shini ya sera dhaifu kama hizi.
ReplyDeleteNafikiri mwisho wa Dunia unakaribia au Mwl. Nyerere atafufuka! Nilifikiri kuwa CHADEMA ndo wangetuletea ukombozi kumbe ndo watadidimiza taifa kiasi hiki? Kwa staili ya kunywa/kuuza gongo tutaleta maendeleo yapi? Nguvu kazi za ya vijana na gongo tangu lini vikaelewana! Kenya walipiga vita pombe za gongo - waone walipo kimaendeleo; Uganda wamehalalisha gongo "maji moto" - waone walipo kimaendeleo! Sasa sisi Wa-Tanzania kama hatuna macho basi tuhalalishe GONGO! Siku gongo ikihalalishwa Tanzania basi mimi binafsi kama Mtanzania sitakuwa na raha ya kujivunia Utanzania wangu!
ReplyDeleteMh...hii hatari!
ReplyDelete