Mwenyekiti
wa Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi Dkt. Rein Zeeman aliyesimama mbele
akiendesha Warsha ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba
juu ya Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi Dkt. Rein Zeeman kushoto akitoa
ufafanuzi kwa baadhi ya Waandishi wa habari
juu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na
Mangariba juu ya Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula
Zanzibar.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Saleh Jidawi katika picha ya pamoja na
Wanachama wa Taasisi ya Interplast baada ya Ufunguzi wa Warsha ya kuwajengea
uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya Kutahiri watoto wa kiume
ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula.
Na Faki Mjaka-
Maelezo Zanzibar 06/03/2014
Taaluma
ndogo katika kutahiri Watoto wa kiume imeelezwa kuwa ni miongoni mwa Vyanzo vya
Ugonjwa wa Fistula ambapo Watoto waliotahiriwa huwa na njia zaidi ya moja ya
kupitishia Mkojo.
Hali hiyo
imepelekea Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi kwa kushirikiana na Wizara
ya Afya kuandaa Warsha ili kukabiliana na tatizo hilo kwa Watoto wa Zanzibar.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Warsha hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Saleh
Jidawi amesema ni vyema Mangariba wakapatiwa mafunzo kutoka kwa Wataalam ili
waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Amesema
kupatikana kwa taaluma ya kutosha kutalifanya tatizo hilo kupungua na kupelekea
Afya za watoto kuimarika.
“Sisi
Serikali kazi yetu ni kuhakikisha
Wananchi wanaondokana na Matatizo ndio maana tukashirikiana na Taasisi
hii ya Interplast ili kuwajengea uwezo Mangariba wetu juu ya tatizo la Fistula”
alisema Dkt. Jidawi.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Interplast Dkt. Rein Zeeman amesema wamekuja
Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu na ushauri ili Mangariba waweze kupata mbinu
bora za kufanya kazi zao.
Amefahamisha
kuwa Jamii inapaswa kuelewa kwamba kazi ya Kutahiri inahitaji kufanywa kwa taaluma
na tahadhari kubwa kama inayochukuliwa katika Upasuaji wa binadamu.
“Jamii
inapaswa kujua kuwa Kutahiri ni jambo la hatari na hivyo linapaswa kufanywa tu
na watu waliopatiwa mafunzo ya kutosha” Alisisitiza Dkt. Zeeman.
Naye Mshauri
wa Taasisi ya Interplast Bi. Ruth Lester amesifia mashirikiano ya kutosha
wanayoyapata kutoka kwa Wananchi na Serikali kwa ujumla.
Ameongeza
kuwa matarajio yao nikuona kazi ya Ungariba haifanywi na kila mtu badala yake
ifanywe na Wataalam waliosajiliwa ili kuepukana na Tatizo la Fistula kwa
Watoto.
Amesema utafiti
waliofanya wamegundua kuwa kila Watoto 1,000 Wakiume waliotahiriwa Zanzibar
wawili hadi watatu wamepata tatizo la Vistula kutokana na kutahiriwa vibaya.
“Tumefanya
utafiti katika sehemu mbali mbali duniani kuhusu kutahiri,kwa mfano Mji wa Birmingham
Watoto 50,000 waliotahiriwa hakuna aliyegundulika na tatizo lakini kwa Zanzibar
kila Watoto 1,000 Wawili hadi watatu wamepata tatizo” Aliongeza Dkt.
Semina hiyo
ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Afya na Mangariba imefanyika Ukumbi wa Hoteli
ya Ocean View mjini Unguja ambapo pia itaendelea katika Kisiwa cha Pemba ili
kuondokana na ugonjwa wa Fistula kwa Watoto Zanzibar.
IMETOLEWA NA
MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment