Habari za Punde

Watanzania waaswa kudumisha na kuuenzi muungano.

                                       Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai .

(Na Jovina Bujulu, MAELEZO DODOMA).
Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar ni jambo la kujivunia kwa watanzania wote na katika bara la Afrika.


Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai wakati wa mahojiano katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC ONE.


Mh. Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kuwa jambo la Muhimu tunalotakiwa kufanya kwa sasa ni kuimarisha na kuboresha Muungano ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo.

“Hatuna budi kuendelea kuuimarisha muungano uliopo ikiwa ni kichocheo cha maendeleo, tumeona mifano kwenye nchi kadha wa kadha zilizo katika muungano mfano nchi Marekani imekuwa mfano bora duniani kimaendeleo hasa kutokana na Muungano uliopo” Alisema Ndugai.

Mh. Ndugai aliongeza kuwa hata Muasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akitukumbusha mara kwa mara kuusimamia muungano wa Tanzania na kuudumisha.

“Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiasa Watanzania wote kuudumisha Muungano wa Tanzania na kuepuka viashiria vyote vinavyoonekana kuvunja muungano, hivyo tushikamane katika kuudumisha”. Alisema Ndugai.

Naye Mjumbe wa Bunge hilo ambaye mjumbe wa secretariati ya marekebisho kanuni za Bunge Maalum Mhesh. Evod Mmanda alisema kwamba miaka 50 ya muungano ni faraja na jambo la kujivunia.

“hatuna budi kwa pamoja kukaa na kuufikiria zaidi Muungano na kutatua changamoto zote zinazojitokeza ili kuudumisha muungano huu na Wasiopenda Muungano  hawana sababu za kutosha” Alisema Mh. Mmanda

4 comments:

  1. kama hayo unayosema ni kweli naomba mfano wa nchi zilituiga muungano , ukiangalia ktk hakuna cnhi zilizoungana kwa mfano wetu badala yake nchi na maeneo mengi yamejitenga kama vile urusi , slovakia , slovenia , kosovo , eritrea , sudani kusini , timor mashariki , na mengineyo mengi , na kwa sasa scotland ipo njiani kujitenga , Muungano hatuutaki msitulazimisheeeeeee mpaka kutufanya tutumie lugha zisizofaa jamaaaaa hheeehhh mmetung'ang'ania kama mavi na........

    ReplyDelete
  2. @Anonymous1.
    1. Kwanza naungana na maoni yako, Sawa sawa maneno yako unayosema, Muungano huu Unaitwa Majina Matakatifu lakini hakuna Nchi hata moja iliovutiwa kuingia katika Muungano huu.

    2. Hawa Watanganyika Kwanini Wanakataa IDENTITY yao na Jina halisi lililounda Muungano huu.?????

    Muungano haukuwa wa Tanzania Bara na Zanzibar bali ulikua wa Tanganyika na Zanzibar.... Hiyo Tanzania isingekuwepo kama sio TAN- + ZAN = TANZANIA..... Sasa watu kama hawa akina MYIKA wanaposema Tanzania Bara wanakua Wanakataa ukweli wa Wazanzibari waliogundua kwamba TANGANYIKA Ndio hiyo Inayojiita TANZANIA BARA... Isipokua imejificha Kaniki la Muungano huo unaoambiwa ni Mtukufu...

    Ninachoona ni Kuwalazimisha Wazanzibari waendelee kutawaliwa na Watu ambao hata janaba hawajui kukoga.. Magovi.... Mwaka huu Mutaitema Zanzibar kwa njia moja au Nyengine....

    ReplyDelete
  3. Miaka khamsini ishapita,zanzibar haijapata maendeleo yanastahiki katika afya,elimu,uchumi,maendeleo ya jamii kwa ujumla.wazanzibari wanaamini iwapo wataachiwa kumiliki maamuzi kuhusu maslahi ya watu wao,basi ufumbuzi utapatikana wa kusukuma gurudumu la maendeleo.wapeni fursa hiyo angalau miaka mitano na baadae watajipanga iwapoambo sio kama walivofikiria.

    ReplyDelete
  4. Inamaana huu muungano kaunda nyerere tu peke yake mbona mnatumia maneno na kauli za nyerere tu na za Karume hamzisemi kama Muungano nikama koti likikubana tu unalivua pumbavu zenu msiotaka nchi yenu TANGANYIKA

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.