Madina
Issa na Khamisuu Abdallah
MTOTO
wa kiume anaekisiwa kuwa na umri wa
miaka sita mkaazi wa Bambi, amepigwa na baba yake kwa kitu kizito na
kumsababishia maumivu makali.
Akizungumza
na waandishi wa habari hizi, Daktari wa kitengo cha mkono kwa mkono cha hospitali
kuu ya Mnazimmoja, Salum Omar Mbarouk, alithibitisha kumpokea mtoto huyo na
kusema dalili zinaonesha alivunjika.
Alisema
baada ya kumpokea alimpima na kugundua kuwa mtoto huyo alipigwa na kitu kizito kilichomsababishia
kuvunjika.
Aidha
alisema mtoto huyo baada ya kupelekwa katika mashine ya kuchunguza mifupa (x-ray)
ilionesha mtoto alivunjika na tayari ameshaanza kupatiwa matibabu.
Hivyo
alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao kwani hao ndio tegemeo
la baadae.
Aliitaka
jamii inapowaokota watoto kama hao
wanaofanyiwa udhalilishaji kuripoti kituo cha polisi ili sheria iweze kuchukua
hatua zaidi.
“Baba
yake ana tabia ya kumuacha mtoto wake nyumbani ambapo huondoka na mtoto wake wa
kike sasa huyu huondoka na kwenda kiambo cha juu kwa ajili ya kucheza lakini
akirudi huchezea kipigo,” alisema Mratibu wa wanawake na watoto, Mashavu
Ramadhan Abdallah,.
Alisema
mtoto huyo alimuona kwa bibi ambae alimuhifadhi baada ya kumuona anapigwa.
Sambamba
na hayo Mratibu huyo alisema baba huyo ni mzoefu wa matukio ya udhalilishaji
kwani alimtahiri mtoto Gumba kwa kutumia kisu huku dawa ikiwa pombe ya kienyeji.
“Baba
yake huyu mtoto anaonesha kuwa ni katili sana
kwani alimtahiri kwa kisu na pombe ya kienyeji kufanywa ndio dawa,” alisema.
Alisema kwa sasa baba mzazi wa mtoto huyo yupo chini
ya ulinzi katika kituo cha polisi Dunga huku mama yake hajulikani alipo.
Nae
mtoto Gumba alisema baba yake huwa anampiga mara kwa mara baada ya kutoka kiamboni kucheza na wenzake.
Binafsi namuonea huruma huyo mtoto inanikumbusha mie mwenye nikiwa Mdogo Baba yangu alikuwa hajuwi kuelimisha yeyey ukifanya kosa ujuwe ni fimbo alikuwa akinipiga mfano wa pweza wakati huo mie bado ni mtoto akili yangu inahitaji Baba kunielimisha na kunieleza ubaya na uzuri wa mambo lakini yeye hakuwa hivyo Baba yangu alikuwa ni mtu wa sala Tano ,nakumbuka ipo siku nikiwa nacheza na wezangu kifungo cha chati kikakatika na kwa kuwa siku hizo unambiwa usiende tumbo wazi mie nikatafuta nijiwe kidogo nikatia ili kuweka kiwe kama kifungo kufika nyumbani hakukuwa na msalie mtumi kiao kule ,nilifika mahali nikawa nipo tayari nimwagie petrol nimuwashe moto lakini sikuwa na uwezo wakuipata hadi hii leo mapenzi yangu kwake ni ile tu Mmungu anatutaka tuwaenzi wazazi na kila nikikumbuka inakuwa najihisi kama jana na kama ingekuwa kipigo chake ni elimu basi sasa ningekuwa namimi na kwenda mwezini
ReplyDelete