Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi kwa kipindi cha robo mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana jioni, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Kwanza Assalaam alaykum.
ReplyDeleteNdugu Othman, blog yako tunaipenda sana kwani inatupa habari nyingi za huko nyumbani. Lakini kitu kimoja, mbona hizi comment zetu na kukutaka kuwa makini katika habari zako huzifanyii kazi. Angalia hapa kichwa cha habari kinazungumzia Mh. Rais kuzungumza na viongozi wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, lakini picha na maelezo ya picha hizo ni za viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria!!
Tumetoa comments nyingi kuhusu hili, hadi wengine wakasema hivi hizi habari hazihaririwi kabla ya kuchapishwa??
Tujiahidi, blog yako iko online hivyo ni kusema inasomwa ulimwengu mzima, makosa madogo kama haya yataipotezea hadhi blog yako tunayoipenda.
Ijumaa karym
Waalaykum Salaam
ReplyDeleteNi kweli mkuu tumeteleza. Tutajitahidi kuwa makini wakati mwengine tuynahitajia comments kama zenu kutuzindua. Shukran mdau endelea kututembelea
Sawa Kamanda Othaman kwa kukubali makosa ndio ubinaadamu, tuzidi kujiweka sawa. Maana sisi wengine huku nje tukiamka tu, basi baada ya kufanya yanayotulazimu basi tena kwanza hufungua Zanzinews kujua nyumbani kuna nini, na tukikosa habari yoyote mpya kutoka Zanzibar kupitia blog hii hujisikia wanyonge kidogo, then huelekea mitandao myengine, hivyo jitahidi kutupashwa habari za uhakika ili tufaidike sisi tulio mbali na home land yetu Zenjjjjjjjjjjjjjjjjjjjjjjiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
DeleteAllaahu mma baarik Zinjibaaaaaaaaaaaaaaar na watu wake amiiiiiiiiiiiiiiiiiiiin.