Na
Kadama Malunde,Shinyanga
Kijana mmoja aitwaye Mihangwa Maguta (30) mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya
Mwadui-luhumbo wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga, ameuawa kwa kupigwa jiwe
kubwa kichwani na wenzake watatu kutokana na kile kilichotajwa kuwa
aliwadhulumu pesa za mauzo ya madini ya almasi.
Kwa
mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kaimu
Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Shinyanga, ACP Kihenya Kihenya, tukio hilo limetokea mwishoni
mwa wiki majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui-Luhumbo
wilayani Kishapu.
Alisema
marehemu aliuawa kwa kupigwa jiwe kubwa
na wenzake kichwani na kumsababishia kifo chake papo hapo.
Kamanda
Kihenya alisema marehemu na wenzake walikuwa wanafanya shughuli ya kuchimba
madini ya almasi katika eneo la mgodi wa madini ya almasi Mwadui unaomilikiwa
na Wiliamson na baada ya kupata madini
walimpa mwenzao akayauze ili wagawane
pesa.
Hata
hivyo, marehemu baada ya kuuza madini hayo aliwadhulumu wenzake na ndipo walipopandwa na hasira wakaanza kumshambulia
kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na alipoanguka chini walibeba jiwe
kubwa kwa pamoja na kumpiga nalo kichwani na kusababisha kifo.
Kamanda
Kihenya alisema thamani ya pesa ya madini haijuliknani kutokana na watuhumiwa
kutokujua thamani yake halisi, huku akitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni
kugombania mali .
Aliwataja
watuhumiwa wa mauji hayo kuwa ni Makoye Mtemi (56), Abdallah Iddi (32) na Ally
Omari (22) wote wakazi wa kijiji kimoja cha Nyenze wilayani humo na
wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi.
No comments:
Post a Comment