Na
Mwandishi wetu
Serekali imeelezea kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Balozi wa Malawi nchini,
Flossie Gomile Chidyaonga,kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.
Balozi
Chidyaonga alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Aga Khan ya hapa Dar
es Salaam.
Taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, imesema
Balozi Chidyaonga aliitumikia serikali ya Malawi katika nyadhifa mbalimbali.
Imesema
kati ya mwaka 2006 hadi 2010 alikuwa Naibu Balozi wa Malawi
nchini Uingereza na baadaye Kaimu Balozi hadi alipoteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini
Tanzanaia.
Taarifa
hiyo imesema siku ya Jumatatu, alishinda vizuri na kufanya shughuli zake kama kawaida.
Hata hivyo,
ilipofika usiku, alijisikia vibaya na kupelekwa hospitali ya Aga Khan, Dar es
Salaam ambapo alipatiwa matibabu na kuwekwa mapunziko kuanzia saa 6 usiku hadi
saa 12 asubuhi aliporuhusiwa na kupewa dawa za kutumia nyumbani.
Balozi
Chidyaonga aliendelea kutumia dawa hizo na hali kuonekana kuimarika hadi siku
ya Ijumaa ambapo aliamka vizuri hadi ilipofika majira ya saa 6 mchana, hali
yake ilipobadilika na kukimbizwa tena hospitali ya Aga Khan ambapo alipokelewa
daktari alisema amekwishafariki.
Mwili wa
marehemu umehifadhiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na uchunguzi wa madaktari
umeonesha marehemu amefariki kutokana na mshipa mkuu wa aorta kuvimba na
kupasuka kulikosababisha damu kukusanyika kwenye mfuko wa moyo na hivyo kufanya
moyo ushindwe kufanya kazi yake.
Leo mwili
wa marehemu utachukuliwa kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupelekwa
ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere ambapo kutafanyika misa ya
kumuombea marehemu na kutoa heshima za mwisho kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Mwili wa
Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Blantyre, Malawi kesho na mazishi
yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano.
Katika
kipindi chote alichokuwa mwakilishi wa Malawi nchini, Balozi Chidyaonga
alifanya kazi yake ya kukuza na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili
kwa umahiri wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment