STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 17 Mei , 2014
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein amesema uhusiano mzuri wa kisiasa na kidiplomasia uliopo kati ya Zanzibar na Vietman unatoa
fursa ya kipekee ya kuuimarisha kwa kupanua maeneo mapya ya ushirikiano kwa
kuhusisha sekta binafsi.
Amesema
Zanzibar inayo mengi ya kujifunza kutoka Vietnam hasa katika sekta za
kilimo, uvuvi na utoaji huduma sekta ambazo zimeifanya nchi hiyo kuwa miongoni
mwa nchi zilizopata mafanikio makubwa ulimwenguni.
Akizungumza na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Nguyen
Phuong Nga Ofisi Kwake Ikulu leo, Dk. Shein alieleza kuwa amefurahishwa na
hatua iliyofikiwa ya mazungumzo ya ushirikiano katika sekta ya kilimo na uvuvi
ambayo ni sehemu ya matokeo ya ziara yake nchini Vietnam Novemba mwaka 2012.
Alibainisha kuwa
matokeo ya timu ya Serikali ya Vietnam
iliyofika nchini kufuatia ziara yake hiyo yataweka misingi madhubuti wa
ushirikiano katika nyanja hizo na hatimae kusaidia kufikia lengo la Serikali la
kujitosheleza kwa chakula hususan mchele kama
lilivyo katika Mkakati wa kujitosheleza chakula nchini.
“Nimefurahi
kusikia kuwa mazungumzo yamefikia hatua nzuri kuhusu ushirikiano kati ya nchi
zetu katika nyanja za kilimo na uvuvi na ninaamini kuwa mazungumzo hayo yatatoa
matokeo mazuri kwa manufaa ya Serikali na wananchi wa nchi zetu” Dk. Shein
alimueleza Naibu Waziri huyo na kuongeza kuwa Zanzibar ina ari kubwa ya
kujifunza kutoka Vietnam ili kufikia azma yake ya kufanya mapinduzi ya kijani.
Sambamba na
ushirkiano katika ngazi za Serikali Dk. Shein alisisitiza kuwa fursa ya
uhusiano huo mzuri ambao umeanza mapema miaka ya sitini haina budi kutumika kwa
kutoa nafasi kwa sekta binafsi za nchi mbili hizo kushiriki katika biashara na
uwekezaji ili kuimarisha zaidi udugu na urafiki kati ya Serikali na wananchi wa
Zanzibar na Vietnam.
Mbali na sekta
za uvuvi na kilimo Mhe Rais alihimiza ushirikiano kati ya nchi hizo katika
sekta ya utalii na huduma ambazo zote nchini Vietnam
zimeonesha kuimarika na kusisitiza kuwa milango iko wazi kwa wawekezaji na
wafanya biashara wa Vietnam
kufanya shughulizi zao Zanzibar .
Dk. Shein
alimueleza Naibu Waziri huyo kuwa ziara yake nchini Tanzania
imedhihirisha urafiki na udugu wa kweli kati ya Tanzania
na Vietnam na kuongeza kuwa Tanzania
ingependa kuona ukaribu wa wananchi wa nchi mbili hizo unaimarika zaidi.
Kwa upande wake
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam Nguyen Phuong Nga alieleza kuwa
Serikali na wananchi wa nchi yake wanajivunia
na kuthamini uhusiano na urafiki wake na Serikali na wananchi wa Tanzania na
kwamba imekuwa bahati kwake kupata fursa kufanya ziara humu nchini.
Kwa hiyo
alisema kuwa kuna kila sababu ya kuimarisha uhusiano huo na kukubaliana na rai
aliyoitoa Mheshimiwa Rais ya kutumia mazingira mazuri ya uhusiano wa kisiasa na
kidiplomasia uliopo kati ua nchi hizo kupanua maeneo ya ushirikiano.
Alibainisha
kuwa ziara yake nchini Tanzania
imelenga katika kuhakikisha kuwa uhusiano kati ya Vietnam
na Tanzania
unaimarika.
Postal Address: 2422 Tel.+255
776 613 015, Fax: 024 2231822
No comments:
Post a Comment