Habari za Punde

Madhara ya mvua : Jumba laporomoka Miembeni, Chake, Pemba

Jumba ambalo liliporomoka katika mtaa wa Miembeni Chake Chake  na kuangukia katika Duka la mfanya biashara  mmoja wa mjini hapo na kusababisha hasara kubwa.


Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Pemba, wakiangalia  Uwezekano wa kuokoa mali iliyoathirika na Kifusi cha Jumba hilo.

Askari wa Kikosi cha Zimamoto Pemba, wakijaribu kuokoa mali na mabaki ya Nyumba hiyo huko katika Mtaa wa Miembeni Chake Chake Pemba.

Mabaki ya Jumba hilo ambalo kwa sasa ni hatari kulitumia kwa kuishi ama kwa makaazi ya watu

Picha na Bakar Mussa -Pemba

2 comments:

  1. Hizi ni Nyumba za zamani ambazo wakiishi au kumilikiwa na Wahindi kabla ya Mapinbduzi... Baadae zikataifishwa na SMZ nakukodishwa au kuuziwa watu binafsi... Nyumba hizi nazifananisha na lile Jumba la pale Darajani ambalo nalo limeoza kabisa kabisa...

    Kazi ya Manispaa ya Mji wa Chake Chake kuzuia watu kutohamia au kukodi majumba hayo mabovu na badala yake yangevunjwa na kujengwa upya.. kiasi cha horofa mbili nakufanywa kama vile shorping mure... Lakini knachoonekana ni Vission ya Baraza la mji ambalo hata kumaliza jumba lake limeshindwa..

    ReplyDelete
  2. Mdau namba 1. Umesema kweli, haya majumba kwa kweli Serikali inapaswa kuangalia upya jinsi ya kuwepo kwake na matumizi ya makaazi ya binaadam. Jumba lile la Train pale Darajani pamoja na kuwa ni sehemu ya hufadhi ya mji mkongwe linapaswa kuangaliwa kabla halijaleta athari kwa wananchi na mali zao.

    Ingependeza kama lingeimarishwa/au kuvunjwa kabisa na kujengwa jengo la ghorofa 2 au 3 kwa ajili wafanyabiashara. Kwa sasa haya majumba yote Unguja na Pemba yanapaswa kukaguliwa upya juu ya umadhubuti wake.

    Tujihadhar kablal athaar.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.