Habari za Punde

Raza akutana na wanahabari


  Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kufutwa jina lake katika ratiba ya ziara ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipotembelea Jimboni kwake jana jambo ambalo hakupendezewa nalo, (kushoto) Afisa habari Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhan Ali.
 
Sehemu ya waandishi waliofika katika Mkutano huo jana Mei 26, uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

2 comments:

  1. Alah ! sasa tuelewe nini jamani.Mbona katika makabidhiano ya madawati kwa skuli ya Mgenihaji ,Raza alikuwepo na mama Sheni pia alikuwepo? sasa imekuwaje.Nini kInachoendelea Raza? Inaelekea ndani ya jimbo lako Raza kuna ufa mzito katika medani ya siasa.

    ReplyDelete
  2. @ Yambayana hiyooooooooo, CCM kwa CCM wanaanza kulana wenyewe.. Mtu Mnafiki ni mnafiki na hua hafiki mbali... Mh. Razza amekasirishwa na kitendo cha Kufutwa jina lake katika Shuhuli zilizofanyika Kitope ambazo Mke wa Raisi na VIP2 ndio waliokua wageni Rasmi kuwatangaza Waume zao katika kwa Wazanzibari...

    Wewe Mh. Razza umekua kama mnafiki, unakumbuka ulivokua ukigomba mpaka ukitaka kulia juu ya Muungano unavoinyanyasa Zanzibar? Na ukafika kusema kwamba Muungano huu utavunjika kama Tanganyika haijajifunua Koti la Muungano?

    Lakini Ulipofika Dodoma Uli-UFYATA Kwiiiii kama wewe Sie.. Na hilo Tu ndio limewafanya Wahafidhuna Mwana Mwema Sheni na Asha Sefu Ali Iddi wakufute katika ziara ya jimbo lako... Sasa uchague kunyoa au Kukata.. Kwani CCM hutakiwa kwasababu ya Rangi yako na Wazanzibari hawana imani nawewe kwasababu ya Unafiki wako....Hata bado naona idhara zimejaa katika nyoyo zenu unafanya mchezo na dhulma wanayofanyiwa Wazanzibari na Waislamu wee.. Dua zao ndio majibu ya hayo yote

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.