Na
Kauthar Abdalla
WAZANZIBARI
12 wanashikiliwa na vyombo vya usalama katika kisiwa cha Madagascar kwa
tuhuma za kuingia nchini humo kwa njia ya haramu.
Watu
hao ambao ni nahodha pamoja na mabaharia 11 wanaofanyakazi katika meli ya
mizigo ya MV Wete inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu visiwani Zanzibar,
Saidi Mbuzi, wanashikiliwa nchini humo baada ya meli hiyo kupata hitilafu za kiufundi wakati ikiwa njiani
kuelekea katika kisiwa cha Mauritius .
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya ndugu na jamaa wa watu hao,
walisema baada ya kuharibika meli hiyo ambayo ilikuwa imebeba mizigo, nahodha
aliamua kutia nanga katika visiwa vya Madagascar kwa ajili ya
matengenezo.
Walisema
wakati wakiendelea na matengenezo walivamiwa na maofisa wa usalama wa Madagascar na
kuwakamata kwa kuingia nchini humo kinyume cha sheria.
Kwa
mujibu wa taarifa za ndugu zao, wananchi hao walisema meli hiyo iliondoka Zanzibar tokea Februari 2 mwaka huu kuelekea Mauritius .
Mmoja
ya watu hao aliyejitambulisha kwa jina la Fatma Hassan Khamis ambae ni mke wa
nahodha wa meli hiyo aliemtaja kwa jina la Amour Ali Juma, alisema alipigiwa
simu na mumewe na kumuarifu kuwa wanashikiliwa nchini Madagascar baada ya meli yao kupata hitilafu.
Mwengine
Mohammed Ali Haji ambae ndugu yake, Haji Ali Haji anashikiliwa huko, alisema
nduguye alimwambia kuwa wametakiwa kulipa fidia yenye thamani ya shilingi
milioni 17 za Tanzania, ili waachiwe huru lakini fedha hizo hawana.
Aidha,
walisema wamechukua juhudi za kumfuata mmiliki wa meli hiyo kuzungumzia sakata
hilo, lakini hadi sasa hawajampata.
Ofisa
kutoka Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) ambae alikataa kutaja jina
lake kwa kuwa sio msemaji wa mamlaka, alisema hakuna taarifa rasmi zilizofikishwa
na mmiliki wa meli hiyo kuhusu sakata hilo .
Nae
mmiliki wa meli hiyo katika mazungumzo kwa njia ya simu na mwandishi wa habari
hizi, alikiri meli hiyo pamoja na mabaharia wake kukamatwa nchini Madagascar, lakini
akasema kuwa suala hilo
amelifikisha serikalini ili kuchukua hatua.
Kuhusu
kufuatwa na ndugu za mabaharia hao, aliwataka kuendelea na subra wakati
serikali ikiendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha ndugu zao wanaachiwa huru.
No comments:
Post a Comment