Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba meja
mstaafu Juma Kassim Tindwa, akizungumza katika hafla ya kukabidhi ujenzi wa
jengo la kisasa la huduma kwa wateja la TTCL Pemba, ambapo mjenzi ni kampuni ya
Ms Quality building Ltd, katikati ni afisa kutoka TTCL na wa mwisho ni mkuu wa
wilaya ya Chakechake, Mwanajuma Majid Abdalla.

Afisa tawala wilaya ya Mkoani, Abdalla
Salim akizungumza na masheha wa wilaya hiyo, hawapo pichani, wakati akifungua
mafunzo ya kuwatambulisha wasaidizi wa sheria wa majimbo, kulia ni mwanasheri wa
afisi ya mkuu wa mkoa wa kusini Pemba, Matar Zahoro na katikati ni Mratibu wa
kituo cha huduma za sheria Zanzibar , tawi la Pemba Fatma Hemed Khamis, ambao
ndio waandaji wa mafunzo hayo yaliofanyika skuli ya sekondari Uweleni.
Wanakikundi cha ususi wa mikoba, makawa,
vipochi vya ukindu na upandaji miti, kilichopo shehia ya Changaweni wilaya ya
Mkoani Pemba, ambao wengi wao ni walemavu, wakiwa katika kazi yao hiyo, ambapo
mkoba mmoja wa kisasa wenye zipu huuzwa kati ya shilingi 15,000 hadi shilingi
12,000.
Sheha wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chake chake Pemba nd:
Salim Ayuob akizungumza na wanajumuia ya ‘Matumaini mapya’ ya wanawake wenye
ulemavu, waliopo Vumba shehiani humo, akifungua mafunzo
ya siku kumi juu ya ufugaji bora, uwekaji kumbu kumbu na utunzaji fedha,
mafunzo yaliofanyika skuli ya Vitongoji.
Mratibu wa mradi wa Usafi wa Mazingira kupitia Jumuia ya uhamasishaji juu ya utunzaji
wa mazingira, kupiga vita madawa ya kulevya na maabukizi mapya ya Ukimwi ya
Jimbo la Kojani, KOYMOCC, Nd:Hamad Hassan, akizungumza kwenye mafunzo ya siku
tatu, yakiofanyika Kojani, katikati ni Afisatawala wa Wilaya ndogo ya Kojani
Nd: Makame Khamis Makame , akifuatiwa na Mwenyekiti wa KOYMOCC Ali Hamad Mussa
Afisa tawala Wilaya ya Chakechake
Rashid Hadidi Rashid, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo, wajumbe wa kamati tendaji wa jumuiya ya ‘TUMAINI JIPYA’ kisiwani Pemba,
mafunzo yaliyofanyika Gombani Chakechake, kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo
Nd:Ali Suleiman Khamis na kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya Nd: Tatu Abdalla
Mselem.
Afisa mdhamini wa shirika la Taifa la
Biashara Zanzibar (ZSTC) Pemba, Abdulmalik Mohamed Bakar, akizungumza kwenye
uzinduzi wa Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira wa Jimbo la Chambani, unaoendeshwa
na Jumuiya ya Kustawisha zao la Karafuu na viungo Pemba ‘JUKAVUPE’, kulia ni
Kaimu Mweyekiti wa Jumuiya hiyo Ali Abdalla Said na kushoto ni Mratib wa mradi
Omar Ali Kombo (Picha na Haji Nassor
Pemba).
No comments:
Post a Comment