Habari za Punde

Bei za Nguo Zanzibar Juu.

Na Mwandishin Wetu. 
WANANCHI mbali mbali wameeleza kusikitishwa kwao juu ya  suala la upandaji wa bei za bidhaa zikiwemo nguo,kwa ajili ya matayarisho ya sikukuu.
Walisema bei za bidhaa aina hiyo katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku bila ya kufahamu sababu kuu za kuongezeka kwa bei hizo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa wanunuzi wa bidhaa hizo Mwanaisha Mgeni Hassan alisema wafanya biashara wengi wameonekana kuuza nguo,viatu  na bidhaa nyengine zinazohitajika katika kipindi cha sikukuu ambapo jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na serikali kuhusu suala hilo.
Alisema hali hiyo inapelekea kutokuwa na imani na serikali pamoja na wafanyabiashara kwa sababu kuna baadhi ya wananchi hawana uwezo wa kununua kiwango hicho ambacho kimezidishwa.
Alisema kuna baadhi wanakuwa na familia kubwa ya kuwahudumia lakini wanashindwa kwa kuwa kila nguo moja inauzwa shilingi 35,000 na shilingi 50,000.
Nae mfanyabiashara wa nguo za watoto wa Darajani Hassan Mussa Hassan alisema ni kweli kwamba bei za nguo zipo juu na baadhi ya wateja wengine wanashindwa kununua kwa kutoweza kumudu gharama hizo.

Aidha alisema sio kweli kama inavyodaiwa kuwa wafanyabiashara wanazidisha bei za nguo kila ifikapo katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani na kusema kuwa bei inayouzwa mwanzo ndio inayouzwa katika kipindi hicho.
Hata hivyo alisema sababu inayowafanya kuuza bei ya juu ni kutokana ununuzi wa dola inakuwa  kubwa na wakifika nje inakuwa imeshuka ndipo wanapoangalia ile thamani halisi ya bei waliyonunulia.

Pia alisema sababu nyengine ni mamlaka ya TRA upande wa Dar-es-Saalam kuwatoza ushuru kwa mizigo inapofika hapo na inapotolewa kuja Zanzibar pia inalipiwa.

1 comment:

  1. Wallahi Nasikitika Jinsi ya Watu wa Nchi za KiaAfrica wasivokua na Imani ..Inapokua Chritsmas na Ramadhani Bei za bidhaa Hufumuka kupita kiasi utafikiri hao Wanaowauzia bidhaa wana Miti ya mpesa mPesa kwamba watachuma majani..

    Serikali ya Zanzibar kutiokua na Bodi yake yakutia na kuchunguza bei pamoja na kutowachukulia haTUA watu wanaojipandishia bei kinyume cha sheria, imeongezea zulma hii ya mfumuko wa bei za vitu..

    Kule Ulaya Wenzetu ikiwa ni karibu na Christmas wao hushusha Bei ya Vyakula, Nguo na kuwa na Compitition ya SALE kila Duka.. Sisi Ngozi Nyeusi Roho mbaya ndio hupandisha Bei mara 3 na tukawakomoa Wanunuaji .. Kuna siku nilipita Dukani kuuliza kichupa cha Jurm yakupakia mkate au Villager nikaambiwa kinauzwa 25000.. Wakati kichupa hicho hakifiki hata 500mg.... Sasa nimekua na mtindo wakupika Jarm ya Stroburry, Blueburry, Rub-barb na Roseburry ili niwaprlekee ndugu zangu kila mwisho wa mwaka...

    Na nia yangu YA KUFANYA REVOLUTION, nikupanda miti hiyo kule nyumbani VISIWANI halafu watu wataweza kuchuma.. Kwani Miti ya Blueburry inaota kama Mikekewa. Ulaya HUOTA WAKATI WA sUMMER NA KULE NYUMBANI MIEZI YOTE INAWEZA KUKUBALI.. ISIPOKUA SIKU ZA KIANGAZI MTU ANAWEZA K

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.