Mwanrafia Kombo na Amina Masoud, MCC
JUMUIYA ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ) umeiomba
serikali kufanya jitihada za makusudi za kuwasomesha wakalimani kwa ajili ya
kuwasaidia wanachama wao.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Jumuiya hiyo, Rashid Ali Mohamed,ofisini kwake Kikwajuni, wakati akizungumza na
waandishi wa hari hizi.
Alisema kuwepo kwa wakalimani
kutawasaidia watu wenye ulemavu kufuatilia matukio mbali mbali yanayotokea
katika jamii.
Alisema lengo la kuanziwa jumuiya hiyo ni
kuwakusanya pamoja watu wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea na
kuwapatia fursa mbali mbali ikiwemo elimu na mikopo.
Alisema fursa nyengine ni kupatiwa
misaada kutoka jumuiya ya wafanyakazi wa kujitolea (VSO) ambapo makao makuu
yake yapo nchini Uingereza katika masula ya kilimo cha mboga mboga.
Pamoja na hayo pia wanakabiliwa na
changamoto mbali mbali ikiwemo mitazamo finyu ya jamii juu ya kundi hilo na kuwapa majina
mabaya ambayo hayafai kuitwa binadamu.
Aidha alisema watu wenye ulemavu hawapati
haki katika vyombo vya sheria na kusababisha kesi nyingi zinazowahusu kufutwa.
No comments:
Post a Comment