Na Mwandishin Wetu.
WANANCHI mbali
mbali wameeleza kusikitishwa kwao juu ya
suala la upandaji wa bei za bidhaa zikiwemo nguo,kwa ajili ya
matayarisho ya sikukuu.
Walisema bei za
bidhaa aina hiyo katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani zimekuwa
zikiongezeka siku hadi siku bila ya kufahamu sababu kuu za kuongezeka kwa bei
hizo.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi mmoja wa wanunuzi wa bidhaa hizo Mwanaisha Mgeni
Hassan alisema wafanya biashara wengi wameonekana kuuza nguo,viatu na bidhaa nyengine zinazohitajika katika
kipindi cha sikukuu ambapo jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba hakuna taarifa
yoyote iliyotolewa na serikali kuhusu suala hilo.
Alisema hali
hiyo inapelekea kutokuwa na imani na serikali pamoja na wafanyabiashara kwa
sababu kuna baadhi ya wananchi hawana uwezo wa kununua kiwango hicho ambacho
kimezidishwa.
Alisema kuna
baadhi wanakuwa na familia kubwa ya kuwahudumia lakini wanashindwa kwa kuwa
kila nguo moja inauzwa shilingi 35,000 na shilingi 50,000.
Nae
mfanyabiashara wa nguo za watoto wa Darajani Hassan Mussa Hassan alisema ni
kweli kwamba bei za nguo zipo juu na baadhi ya wateja wengine wanashindwa
kununua kwa kutoweza kumudu gharama hizo.
Aidha alisema
sio kweli kama inavyodaiwa kuwa
wafanyabiashara wanazidisha bei za nguo kila ifikapo katika kipindi cha mwezi
mtukufu wa ramadhani na kusema kuwa bei inayouzwa mwanzo ndio inayouzwa katika
kipindi hicho.
Hata hivyo
alisema sababu inayowafanya kuuza bei ya juu ni kutokana ununuzi wa dola
inakuwa kubwa na wakifika nje inakuwa
imeshuka ndipo wanapoangalia ile thamani halisi ya bei waliyonunulia.
Pia alisema
sababu nyengine ni mamlaka ya TRA upande wa Dar-es-Saalam kuwatoza ushuru kwa
mizigo inapofika hapo na inapotolewa kuja Zanzibar
pia inalipiwa.
Wallahi Nasikitika Jinsi ya Watu wa Nchi za KiaAfrica wasivokua na Imani ..Inapokua Chritsmas na Ramadhani Bei za bidhaa Hufumuka kupita kiasi utafikiri hao Wanaowauzia bidhaa wana Miti ya mpesa mPesa kwamba watachuma majani..
ReplyDeleteSerikali ya Zanzibar kutiokua na Bodi yake yakutia na kuchunguza bei pamoja na kutowachukulia haTUA watu wanaojipandishia bei kinyume cha sheria, imeongezea zulma hii ya mfumuko wa bei za vitu..
Kule Ulaya Wenzetu ikiwa ni karibu na Christmas wao hushusha Bei ya Vyakula, Nguo na kuwa na Compitition ya SALE kila Duka.. Sisi Ngozi Nyeusi Roho mbaya ndio hupandisha Bei mara 3 na tukawakomoa Wanunuaji .. Kuna siku nilipita Dukani kuuliza kichupa cha Jurm yakupakia mkate au Villager nikaambiwa kinauzwa 25000.. Wakati kichupa hicho hakifiki hata 500mg.... Sasa nimekua na mtindo wakupika Jarm ya Stroburry, Blueburry, Rub-barb na Roseburry ili niwaprlekee ndugu zangu kila mwisho wa mwaka...
Na nia yangu YA KUFANYA REVOLUTION, nikupanda miti hiyo kule nyumbani VISIWANI halafu watu wataweza kuchuma.. Kwani Miti ya Blueburry inaota kama Mikekewa. Ulaya HUOTA WAKATI WA sUMMER NA KULE NYUMBANI MIEZI YOTE INAWEZA KUKUBALI.. ISIPOKUA SIKU ZA KIANGAZI MTU ANAWEZA K