BAADA ya wamiliki wa shamba lililotumika kuzika watu waliofariki katika
ajali ya meli ya Mv.Skagit kulalamika kuporwa shamba lao liliopo Kama, hatimae
serikali imesema itawalipa shamba jengine katika eneo la Selemu.
Shamba hilo kabla ya kuchukuliwa na serikali lilikuwa limetolewa wakfu na
marehemu,Sultan Ahmed Mohamed El –Mugheriy.
Maiti za ajali hiyo zililazimika kuzikwa katika shamba hilo baada ya
makaburi ya Mwanakwerekwe kujaa huku serikali ikipanga maiti za ajali hiyo
kuzikwa eneo moja.
Ahadi ya kulipa fidia ilitolewa na Mkurugenzi wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi
Maji na Nishati January Fusi, alipokuwa akizungumza na gazeti hili ofisini
kwakwe Forodhani.
Alisema suala la kukubali au kukataa eneo ambalo serikali itafidia litabaki
kuwa la wamiliki.
Hata hivyo, wamiliki wa shamba hilo walisema bado hawajapewa taarifa ya
kufidiwa shamba hilo.
Alisema serikali inafahamu na inaheshimu sheria za Wakfu lakini kutokana na
dharura iliyojitokeza isingekuwa na eneo jengine kwa ajili ya kuwazika watu
hao.
Aidha alisema kwa kuwa sehemu ya
shamba hilo pia limeshachukuliwa na JKU, isingekuwa busara kwa wamiliki
kuendelea kulitumia badala yake ni vyema wakakubali kupokea shamba watakalopewa
na serikali.
Mmoja wa warithi wa marehemu,Qussay Juma Mugheir, alisema kitendo cha JKU
kuvamia shamba lao hakikuwaridhisha kwa sababu hawakujulishwa.
Alisema JKU walivamia shamba hilo tokea serikali ya awamu ya tano na
uvamizi huo unaendezwa na serikali za wamu awamu zote.
“Hali hii imekuwa ikiendelea katika awamu zote ambapo pamoja na kupeleka
barua Kamisheni ya Wakfu na mali ya Amana,Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu,i
mpaka hivi sasa hakuna majibu yoyote tuliyojibiwa,” alisema.
Alisema
wanakusudia kuifungulia mashtaka serikali kwa kitendo cha kuvamia ardhi yao
bila ya ridhaa ya
Hii habari kaka Othman Mapara mbona haijakamilika? imekatika hapo mwisho, tafadhali kama ipo habari kamili tuwekee
ReplyDelete