Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dar-Es-Salaam
Tanzania
Kwa heshima
tafadhali husika na mada ya hapo juu.
Wananchi wengi ndani
na nje ya nchi kwa kupitia vyombo vya habari vinavyoaminika nchini Tanzania
wamepokea kwa mshtuko mkubwa sana habari za kuhuzunisha kuhusu madhila na
vitendo vya kishenzi vya udhalilishaji walivyofanyiwa Watuhumiwa wa Kesi ya Ugaidi
waliokamatwa usiku wa manane nchini Zanzibar na vyombo vyako vya Dola na kuonekana
baadae wakipandishwa kwenye Mahakama ya Kisutu iliyopo nchini Tanganyika.
Watuhumiwa wakiwemo Masheikh wakubwa wenye kuheshimika katika Jamii walilalamika
Mahakamani kwamba walifanyiwa mateso makubwa na vitendo vya kuwadhalilisha
vinavyokwenda kinyume na Haki za Binaadamu kama kuwanajisi na kuwatia majiti na
chupa kwenye sehemu zao za siri za nyuma.
Jumuiya yetu imeshtushwa sana kuona katika
karne hii ya ishirini na moja chini ya Uongozi wako, Serikali yako inaweza
kuwatendea Wananchi wake vitendo kama hivi vya udhalilishaji. Tanzania imekuwa ikijinata
kuendeshwa kwa kufuata utawala wa sheria na kuheshimu haki za Binaadamu, lakini
kadhia ya Masheikh na matukio ya udhalilishaji waliofanyiwa yametuthibitishia
kinyume chake. Jumuiya yetu na wapenda haki wote sio tu tumeshtushwa na matendo
ya kinyama ya vikosi vyako lakini pia tumefadhaishwa na utaratibu mzima
uliotumika kuwakamata watu usiku usiku nchini Zanzibar kwa tuhuma za ugaidi na kuja
kuwafanyiwa mateso na kuwafunguliwa kesi nchini Tanganyika. Hali hii inaonyesha
dhahir shahir jinsi Tanganyika kila kukicha inavyozidi kuidhibiti na
kuzikandamiza Mamlaka za nchi ya Zanzibar. Tumeona kwa mfano, Watu waliokamatwa
Arusha kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya kigaidi, mashtaka yao yalifanyika
mjini Arusha, lakini wale waliokamatwa nchini Zanzibar wamefunguliwa mashtaka
Dar Es Salaam, nchini Tanganyika, ilhali Zanzibar ina Mahakama zenye uwezo wa
kusikiliza kesi kama hiyo waliyoshtakiwa Watuhumiwa.
Jumuiya ya
MUWAZA imewahi kulalamika kwako mara kadhaa juu ya namna ya vyombo vya dola vya
Tanzania vinavyovunja haki za Binaadamu na kuitia dosari nchi lakini tunaona
hali inaendelea kuwa vile vile au tunathubutu kusema inaongezeka kuwa mbaya
zaidi.
Ikumbukwe, kwamba
kwa mujibu wa sheria ya nchi Mtuhumiwa yeyote huwa hana makosa hadi pale
Mahakama itakapothibitisha kwa ushahidi wa kutosha na kumtia hatiani. Hata hivyo, Serikali na Vyombo vyake vya Dola
haina haki kwa njia yoyote ile kutumia vitendo vya utesaji na udhalilishajikwa
Wananchi wake. Kwahivyo, Mtuhumiwa/Mwananchi yoyote anatakiwa Utu wake
uheshimiwe kwa namna zote maana Utu wa kila Mtanzania haugawiki na ni adhimu
. Kumnyima Mtanzania yeyote Utu wake ni
kulinyima Taifa Utu wake na kulidhalilisha mbele ya macho ya Walimwengu.
Kwa mantiki hiyo Jumuiya ya MUWAZA
inakuomba kuliingilia kati suala hili kwa haraka na kuwachukulia hatua wale
wote walioshiriki vitendo hivi viovu vya udhalilishaji vyenye kuvunja haki za
Binaadamu.
MUWAZA
inatarajia barua hii utaipa mashirikiano makubwa.
KATIBU
Jumuiya ya MUWAZA
UK
Nakala: Rais
wa Zanzibar.
Makamo
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Waziri
wa Mambo ya Ndani – Tanzania.
Balozi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania – UK.
Balozi
wa Kenya – UK.
Balozi
wa Rwanda – UK.
Balozi
wa Uganda – UK.
Balozi wa
Burundi – UK.
hii Uk =K ina maana gani
ReplyDeleteUK maana yake ni nini Mh. Katibu
ReplyDeleteUK- Maana yake ni UNITED KINGDOM.
ReplyDelete