Na Mwandishi wetu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi
mbali mbali za serikali ili kujaza nafasi zilizo wazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk.
Abdulhamid Yahya Mzee, walioteuliwa ni pamoja na CRD Juma Haji Juma kuwa Mkuu
wa utawala kikosi maalum cha kuzuia magendo (KMKM).
Uteuzi huo ulifanywa chini ya kifungu cha
53 cha katiba ya Zanzibar
ya mwaka 1984.
Aidha Dk. Shein amemteua Meja Yussuf
Khamis Yussuf kuwa Mkuu wa Utawala KVZ.
Wengine walioteuliwa ni Kanali Ali
Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa utawala JKU, SACP Ali Abdulla Ali kuwa Naibu
Kamishna wa chuo cha mafunzo, Abdulla Ali Ussi kuwa ofisa mdhamini Shirika la
Biashara Pemba kuchukua nafasi ya Abdulmalik Mohamed Bakari ambaye atapangiwa
kazi nyengine.
Wengine ni Sharifa Khamis Salim
alieteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar (BTMZ) na Abdalla
Suleiman Abdalla kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Utawala wa Umma, Zanzibar .
Uteuzi wa watendaji hao ulianza Julai 16,
Agosti 11, 12, 14 na 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment