Habari za Punde

Gemu ninayoikumbuka : Pan African v KMKM 1982


Kutoka kwa Mdau

Katika mechi za mpira wa miguu ambazo bado nina kumbukumbu yake vizuri tu ni mchezo mkali uliofanyika mwaka 1982 kati ya KMKM ya Zanzibar na Pan African ya Dar.

Gemu hii ilipigwa katika Uwanja Amaan mjini Zanzibar katika kugombania ubingwa wa Tanzania wakati ulee ambapo kulikuwa na ligi ndogo inayojumuisha mshindi wa kwanza na wa pili wa ligi ya  Tanzania Bara na Zanzibar ambao hukutana na kucheza mechi za mzunguko na hatimaye kupata wawakilishi wawili waliotuwakilisha katika  kombe la klabu bingwa na kombe la washindi kwa wakati huo.

Ilikuwa ni kipindi pekee ambacho huwa tunabahatika kuziona timu za bara na Zanzibar zikibadilishana viwanja katika kuwania ubingwa halisi wa Tanzania. pia kuwaona wachezaji wengi kutoka bara ambao kwa wakati huo tulikuwa tukiwasikia tu kwenye redio na kuwasoma kwenye magazeti. Pia ilikuwa ni changamopto kwa timu za Zanzibar kuwerza kupata upinzani wa aina nyengine wa soka.

Mechi imebaki katika kumbukumbu yangu kutokana na aina ya kandanda iliyochezwa siku hii na jinsi ya mwenendo wa mchezo wenyewe.

Timu ya KMKM iliyokuwa chini ya Kocha Marehemu Mzee Kheri aliamua kuipanga kama hivi ifuatavyo kama kumbukumbu yangu bado ipo sahihi:

Golini Ramadhan Korosheni, Beki wa kulia ni Abdullah Maulid, Beki wa kushoto alikuwa ni Hassan Mrisho(Zitto) Mabeki wa kati walikuwa ni Ibrahim Kapenta na Mohammed Rajab Kiungo mkabaji aliekuwa akijua kukaba hasa alikuwa na Mohammed Kombo ( Msomali) na kiungo mshambuliaji alikuwa Marehemu Ali Issa (Kapteni) Pembeni alikuwepo Mcha Khamis ( baba yake Khamis Mcha wa Azam) na upande wa pili alikuwepo Said Hamad, Katikati safu ya ushambuliaji kulikuwa na Mohammed Kidevu ( Sheha wa Tomondo kwa sasa) na Shaaban Ramadhan ( Kocha kwa sasa).

Timu ya Pan African ilipangwa hivi, Golini Juma Pondamali (Mensah), beki wa kulia Mohammed Mkweche, kushoto Jaffar Abdulrahman, mabeki wa katikati walikuwa Jella Mtagwa na Leonard Tenga kiungo alikuwa  Mohammed Adolf Rishard na Kassim Manara  ila safu ya ushambuliaji ilikuwa ni Godian Mapango winga wa kulia Mohammed Yahya ( Tostao) Ali Katolila na Peter Tino Winga ya kushoto.

Mchezo ilianza taratibu huku kila timu ilikuwa ikiusoma mchezo wa timu pinzani . Lakini uwezo mkubwa uliooneshwa na timu zote mbili katika kumiliki mpira na kutoeleana mapande ya uhakika ndio jambo lililonifanya nisiusahau mchezo huu.

Pan African walikuwa wa kwanza kuandika bao la kwanza liliwekwa kimiani na Ali Katolila  wakati mvua ikinyesha kitu ambacho kilikuwa cha ajabu siku hiyo kwani kila ikinyesha mvua Pan walikuwa wakiandika bao. KMKM wakapapatua na kuwasazisha bao lilifungwa na Mcha Khamis.  Mvua ikasimama na iliponyesha tena Pan African wakaweka bao la pili mfungaqji Mohammed Yahya “Tostao”. Mvua ikasimama na gemu kuendelea hadi Shaaban Ramadhan aliposawazisha na kufanya matokeo 2-2 nadhani hadi mapumziko.

Kipnidi cha pili ambapo KMKM walikuwa wakicheza mpira wa uhakika waliofundishwa darasani na Mzee Kheri walijitahidi kutandaza kandanda safi lakini walishtukizwa na mabao mawili ya haraka haraka yaliyowekwa wavuni na Peter Tino na Mohammed Yahya Tostao baada ya kupokea krosi maridhawa kutoka kwa Ali Katolila na kupiga Bullet header iliyomshinda kipa Korosheni. Na hadi kumalizika kwa mchezo Pan African 4 KMKM 2

Ingawa KMKM walikubali kipigo lakini kwa waliobahatika kuwepo uwanjani siku hii mimi nikiwa mmojawapo niliridhishwa kabisa na viwango vya timu zote mbili vya uwezo wa kuumiliki , kutoa pasi zenye macho, kujihami kwa pamoja, na magoli yaliyofungwa bado vipo fresh licha ya kupita zaidi ya miaka 30!

Je una gemu yoyote ya zamani unayoikumbuka? Turushie 

4 comments:

  1. mdau kidogo kwenye kumbukumbu zangu huyu (msomali)alikuwa omar kombo na sio mohammed kombo otherwise uko sawa nimeipenda hii

    ReplyDelete
  2. Na hapa kidogo nakuweka sawa peter tino alicheza number 10 na winger ya kushoto ni Ibrahim kiswabi!

    ReplyDelete
  3. hiyo game sio kmkm no small simba n.a. oan

    ReplyDelete
  4. Kikosi Cha Pan African hakikuwa hicho

    Adolf
    Pondamali
    Jafar AbdulRahman
    Tenga

    hawakuwepo

    Kikosi kilikuwa kama ifuatavyo

    1) Ali Yusuf
    2) Mkweche
    3 ) John Faya
    4) Rashid Idd Chama
    5) Jellah Mtagwa
    6) Salum Mwinyimkuu Carlos
    7) Tostao
    8) Hussein Ngulungu
    9) Abdallah Burhan
    10) Ali Katolila
    11) Peter Tino

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.