Na Mwanrafia
Kombo, MCC
VIONGOZI wa
jimbo la Makunduchi wametakiwa kubuni miradi ya maendeleo, licha ya kuwepo kwa
mafanikio makubwa jimboni humo ikiwemo kupatiwa ufumbuzi kwa tatizo la maji safi na salama.
Wito huo
ulitolewa na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi, Mhe. Haroun Ali Suleiman wakati
akizungumza na masheha wa shehia za Makunduchi.
Alisema
miradi ya maendeleo bado inahitajika katika jimbo hilo
ili kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili wananchi wa jimbo hilo .
Aliwataka
wananchi jimboni humo kuendelea kuitunza miradi waliyonayo ikiwemo ya maji safi na salama ili
kutufaika kwa mda mrefu.
Mhe. Haroun
alieleza endapo kutakuwa na miradi ya uhakika na kuendelezwa kama
ilivyokusudiwa, itaweza kumaliza matatizo yanayowakabili wananchi hao sambamba
na jimbo hilo
kupiga hatua kimaendeleo.
Kwa upande
wao Masheha wa shehiya hizo walisema watakuwa mstari wa mbele kusimamia na
kuendeleza miradi hiyo ili kuhakikisha wanaondokana na tatizo la utegemezi.
Nae Afisa wa
Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA), Nd. Zahor
Suleiman alielezea kuwa sehemu nyingi za Makunduchi zimeshapatiwa ufumbuzi wa
tatizo la maji safi
na salama na kuongeza kuwa ni maeneo machache ambayo yanatarajiwa kukamilisha
si muda mrefu.
No comments:
Post a Comment