Na
Laylat Khalfan
KAMISHENI
ya Utalii Zanzibar, imefanya zoezi la kuzichunguza hoteli zote za Unguja na Pemba pamoja na kuzipandisha daraja zilizostahili ambapo
jumla ya hoteli 74 za kitalii zimepandishwa daraja kuanzia la pili hadi la tano.
Afisa
anaeshughulikia viwango vya mahoteli Zanzibar ,
Hassan Burhan wakati akizungumza na Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake
Amani Wilaya ya Mgharibi Unguja alisema zoezi hilo lilikagua hoteli 106 kwa hatua ya awali.
Alisema
kati ya hizo 74 zilipandishwa daraja
tano miongoni mwao 70 kutoka Unguja na 4 Pemba
ambapo upandishwaji wa madaraja hayo ulikwenda kwa mujibu wa vigezo vya Afrika
Mashariki.
Aidha
alisema zoezi hilo litakuwa endelevu na linalenga kubadili mwonekano wa awali
wa hoteli kulingana na mahitaji ya ulimwengu ili kumudu ushindani wa biashara na kuiwezesha Zanzibar kupokea wageni wa
daraja la juu katika kufaidika na sekta ya utalii.
Alisema
miundombinu mibovu kwa baadhi ya hoteli za kitalii imekuwa ikikimbiza watalii
matajiri nchini kutona na kukosekana kwa viwango vinavyostahili, jambo
linalorudisha nyuma ongezeko la pato la nchi.
Akitaja
vigezo vilivyozingatiwa ni pamoja na ubora wa majengo, kuwepo kwa huduma ya
usalama na uhifadhi wa mizigo kwa wageni, vifaa vya kuwahudumia ikiwemo vyakula
na lugha nzuri.
Alifahamisha
hoteli yenye viwango zitatoa huduma ya vyeti maalum vitavyosaidia kujitangaza
na kupata wageni kufuatia huduma bora wanazozitoa sambamba na hilo alihimiza
umuhimu wa wamiliki wa hoteli hizo kufuata mfumo wa kisasa ili kufaidika na
sekta ya utalii wa daraja la juu kama ilivyo kwa nchi nyengine za Afrika
mashariki.
No comments:
Post a Comment