Na Amina Masoud, MCC
MKURUGENZI wateja kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Nd.
Mussa Ramadhan Haji ameishukuru Kampuni ya Japan International
Cooperation
Agency (JICA), kwa misaada inayowapatia.
Mkurugenzi Mussa aliyasema hayo baada ya Kampuni hiyo kupitia
walimu wa taaluma kutoka Japan
kuwatembelea kwa lengo la kukagua miradi inayoendesha na Mamlaka hiyo.
Alisema JICA kwa miaka mingi inaisaidia Zanzibar kupitia mamlaka ya maji Zanzibar
(ZAWA) kwa kuwapatia miundombinu ya maji ya uhakika.
Katika ziara hiyo, Walimu hao walitembelea ZAWA na kujionea
jinsi misaada waliyoitoa inavyofanyakazi na kuwafikia walengwa.
Alisema ugeni huo uliambatana na ziara ya kutembelea visima
vilivyojiengwa kwa udhamini wa kampuni hiyo ili kujua namna vinavyosaidia
wananchi.
Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea chemchem ya maji iliyopo
Mtoni, tangi la maji lililopo Dole Wilaya ya Magharib lenye uwezo wa kuhifadhi
maji lita milioni moja na laki mbili na huyasambaza katika wilaya ya Magharibi
Unguja.
Maeneo mengine waliyotembelea ni pamoja na visima vya maji Welezo
venye uwezo wa kuhifadhi maji zaidi ya lita milioni nne, tenki la kinuni
lenyeuwezo wa kuingiza maji milioni mbili na laki saba pia walifika kwenye
tangi kubwa la maji Saateni.
Aidha Mkurugenzi Mussa alieleza ujio wa ugeni huo ulikuwa na lengo
la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya watu wa Zanzibar
na Japan ambapo pia kampuni hiyo inatarajia kujenga soko la kushushia na kuuzia
samaki kutoka Japan ,
sambamba na kuchukua baadhi ya Wazanzibai kwenda kusoma Japan ili
kazidisha uhusiano wao.
Alieleza mradi huo ulioanza tokea mwaka 2006 umetenga fedha
taslimu za kutaka kuiisaidia mamlaka ya maji ZAWA ili kuendeleza shuhuli zake
za kuwasaidia wananchi, sambamba na kuboresha miundo mbinu ya maji nchini.
No comments:
Post a Comment