Habari za Punde

Mtoto wa miaka 9 abakwa, auawa

Na Kadama Malunde, Shinyanga
MATUKIO ya ukatili dhidi ya watoto yameendelea kujitokeza mkoani Shinyanga ambapo mtoto wa miaka 9 ambae ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika skuli ya msingi Negezi iliyopo kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga, ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa macho.

Tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi tarafa ya Shinyanga mjini, ambapo mtoto huyo alikutwa kwenye kichaka vilivyo karibu na shamba la Mwandu Misona.

alioshuhudia tukio hilo walisema mtoto huyo alikutwa akiwa amefariki dunia huku mwili wake ukiwa umetobolewa sehemu mbali mbali.


Akielezea zaidi kuhusu tukio hilo baba mazazi wa mtoto huyo Kashindye Mayala alisema mwanawe alikuwa anaishi na shangazi yake Mahegi Mayala na aliaga kwenda kunyoa nywele saluni majira ya saa tisa alasiri siku ya Jumapili na baada ya hapo hakurudi tena nyumbani.

Alisema siku ya Jumatatu walipata taarifa kuwa kuna mtoto ametupwa vichakani karibu na shamba la Mwandu Misona na walipofika eneo la tukio hawakumkuta mtoto huyo na kudaiwa kuwa amepelekwa na wasamaria wema hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Alisema kufuatia taarifa hizo aliamua kuufuatilia mwili huo hospitalini hapo,ili kubaini kama ni mtoto wake na alipofika chumba cha kuhifadhia maiti alibaini mwili huo kuwa ni wa mtoto wake.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga, Dk. Daniel Maguja, alisema waliupokea mwili wa mtoto huyo Agosti 25, mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni na kuongeza kuwa vipimo vilionesha mtoto huyo alibakwa na kutobolewa.


Kamanda wa polisi mkoani, Shinyanga SACP Justus Kamugisha, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa chanzo kinachunguzwa ili kuwabaini wahusika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.