Na Kadama
Malunde,Shinyanga
CHAMA cha Alliance for
Change and Transparency (ACT), kimewataka Watanzania kuacha kutumiwa na
wanasiasa kama daraja la kufikia mafanikio.
Kimesema baadhi ya
viongozi wa siasa wanawatumia Watanzania kujinemesha,huku wao wakiendelea kubakia katika dimbwi la umasikini.
Aidha kimesema muda
umefika wa kuleta mabadiliko na kuweka wazi kuwa ACT hakina mpango wa kuunga
mkono CCM.
Akizungumza na wananchi
wa manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya
mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini,Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Kadawi
Limbu,aliwataka wananchi kuwapuuza wanaosema wao ni CCM B.
Limbu alitumia fursa
hiyo kuwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa na kuchambua kwa kina kauli zao wanazozitoa
majukwaani,kwani wengi wao wanatafuta njia ya kujineemesha na hawana uzalendo
na nchi yao.
“Ndugu zangu, ACT siyo
CCM B na wala hatuna mpango wa kuunga mkono CCM, hiki ni chama kipya kimeletwa
kuwakomboa Watanzania,”alisema.
Naye Katibu wa vijana
ACT Taifa, Philip Malack, alisema wanataka kuwaunga mkono Watanzania
wanaopigania haki na kuomba kuwapa
ushirikiano, ili kufichua maovu yaliyojificha.
Alisema wapo vigogo
kutoka vyama vingine vya siasa watakaojiunga na ACT hivi karibuni.
Alisema huo ni uzinduzi
wa mkutano wa kwanza wa ACT kanda ya ziwa na kubainisha kuwa wataendelea
kutembelea mikoa yote ili kufikisha ujumbe kwa Watanzania na
kujitambulisha,huku akivitaka vyama vya upinzani kuacha kupotosha wananchi juu
ya chama hicho.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa ACT mkoa wa Shinyanga, Justina Kimisha, alisema chama hicho kimeweka
mikakati ya kuleta mabadiliko tofauti na vyama vingine.
Aliwaomba wananchi
kushiriki kikamilifu kwenye mikutano ili waone tofauti iliyopo na vyama
vingine.
No comments:
Post a Comment