Na Magreth Kinabo,
Dodoma
CHAMA cha Wakulima
wadogo wa pamba Tanzania (TACOGA),
kimemwomba Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, kusitisha mchakato wa bunge maalum la katiba.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu chama hicho,
George Mpanduji, wakati
akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge
maalum la katiba, Samuel Sitta,ofisini mjini Dodoma.
Mpanduji alieambatana na baadhi wa viongozi na wajumbe
kutoka mikoa 11 wa TACOGA ,alisema
wanaheshimu makubaliano ya kisiasa ya kutungwa katiba,lakini wana hofu
kwamba katiba hiyo haitapatikana.
Aidha alishauri agenda
za haki za jamii zipewe kipaumbele kwa
kuwa kuna vilio vya kuhitajika suluhu za haraka baina ya jamii moja na
nyengine.
Alisema wakulima
wanataka katiba ipatikane haraka kwani itakuwa suluhisho dhidi ya mizozo na
wafugaji, lakini wana hofu kwama azma hiyo inaweza kushindikana.
Kwa upande wake Sitta
alisema lengo la bunge hilo ni kutunga
katiba iliyo rafiki yenye kukidhi matakwa ya wananchi.
No comments:
Post a Comment