Na Mwandishi wetu
VIJANA wawili wameuawa
kinyama baada ya kuchomwa moto wakiwa hai katika eneo la Tabata Liwiti
wakituhumiwa kuiba pochi la mwanamke.
Walioshuhudia tukio hilo
walisema,limetokea mwishoni mwa wiki ambapo baada ya kukwapua pochi hilo
walikimbia na kuanza kufukuzwa.
Walipokamwa walipigwa
vibaya na kisha kuchomwa moto hadi kufa.
"Matukio ya
waendesha piki piki kukwapua yamekuwa
yakitokea mara hapa Tabata na wanapokamatwa na wanapigwa na baadae kuchomwa
moto kwa sababu wanapopelekwa vituo vya polisi wanaachiwa,” alisema mwanamke
mmoja.
No comments:
Post a Comment