Na
Benedict Liwenga, Maelezo
Masuala ya migogoro ya ardhi inayowahusisha wafugaji na wakulima na uraia pacha,
yamerejea tena katika mjadala wa katiba mpya unaoendelea Dodoma.
Masuala
mengine yaliyochukua nafasi ni haki ya afya, haki ya kuishi ikiwemo sheria ya
kunyonga, haki za binadamu, haki ya mtuhumiwa na mfungwa, haki za wafanyakazi
na ajira pamoja umri katika ajira pamoja haki za vijana.
Mjumbe
wa kamati namba sita,Zaina Madabida, alisema ni vyema kuwepo kwa kipengele
kinachotambua mila na desturi za makundi ya wafugaji na wakulima ili kuondoa
migogoro ya ardhi ambayo inajitokeza mara kwa mara.
Kuhusu
haki ya kuishi pamoja na sheria ya kunyonga, alisema sheria ya kunyonga ni
vyema iendelee kuwepo katika kikatiba.
“Adhabu
ya kifo iendelee kuwepo kama katiba yetu ya sasa inavyosema kwani kuna watu wao
wamekuwa na tabia za kuwaua wenzao,” alisema.
Kuhusu
haki za binadamu, alisema maoni ya wachache yamefafanua kuwa haki ya kuishi
ianzie tangu pale mimba inapotungwa kwani siku hizi watu wengi wamekuwa na
utaalamu katika kutambua viumbe vilivyomo tumboni.
Alisema
ibara ya 39 inayohusu haki ya mtuhumiwa na mfungwa, kamati yake imeitaka katiba
izingatie mazingira rafiki kwa watuhumiwa wenye ulemavu.
Mjumbe
wa kamati namba 10, Monica Sophu, alisema masuala ya ardhi yamekuwa na
changamoto nyingi na ni vyema ikaundwa Tume Huru ya Ardhi ambayo itakuwa na kazi
ya kushughulikia migogoro hiyo.
Kuhusu
haki za vijana, mjumbe Jesca Msavatavangu, alisema haki hizo hazijaainishwa vyema
na kushauri katiba iainishe haki zaote za vijana.
Kuhusu
uraia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema sura ya 56 inayohusu suala la
uraia ni vyema likaangaliwa kwa umakini mkubwa.
Aidha
alipendekeza uraia wan chi moja kwa sababu Tanzania bado haijaweza kujilinda
vya kutosha.
“Watu
watatumia fursa ya uraia pacha kuhujumu uchumi wetu, kwani kuna mazingira mengi
ya rushwa, hivyo suala la hili lije kufikiriwa baadaye sana sio sasa hivi,” alisema.
No comments:
Post a Comment