Na
Fatina Mathias, Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, amesema rasimu ya mwisho itakamilika
Septemba 21 mwaka huu ambapo wajumbe wa bunge hilo watakuwa wamefikia lengo
walilowekewa na taifa la kutoa katiba.
Akizungumza
katika bunge hilo, Sitta alisema katika kikao cha jana (juzi) cha Kamati ya
Uongozi, wamedhihirisha kwamba wanakwenda vizuri na Kamati ya Uandishi ambayo
imekuwa ikitazama mambo yanavyokwenda, imejipanga kutoa rasimu ya mwisho
Septemba 21.
“Ratiba
yetu ya bunge maalumu inaendelea kama ilivyopangwa,siku 60 za bunge hili ambazo
ni nyongeza ya siku tulizopewa kwa
mujibu wa sheria zinaishia Oktoba 4,”alisema.
Aidha
alisema akidi inahusu wajumbe wote ambao waliteuliwa na Rais kuwa wajumbe wa
bunge hilo.
Alisema
sekretarieti imeandaa muhtsari wa maoni yalivyotoka ndani ya kamati 12, kwa
maana hivyo mwenendo wa ndani ya bunge maalum hautaibua mjadala mpya.
Aidha
alisema baadhi ya wajumbe katika kamati zao wamerejea tena kuidai Mahakama ya Kadhi
ndani ya katiba na wengine wanasema ndivyo ilivyo Uganda wakati sio kweli.
Aliwaomba
wajumbe kutorudia tena yale yaliyojadiliwa kwenye kamati na kwamba hoja
ikashindikana iwekwe pembeni.
No comments:
Post a Comment