Na Joseph Ngilisho, Arusha
KAMANDA wa Kikosi cha Kuzuia na
Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (SACP) Godfrey Nzowa, ameapa kutokomeza
wimbi la uingizaji na usafirishaji wa dawa za kulevya huku akisisitiza
kupambana na vigogo wanaotajwa kuhusika
na mtandao huo.
Alitoa wito kwa jamii kuunga
mkono jitihada zake za kupambana na mtandao huo, aliodai ni hatari, kwa kutoa
taarifa za siri ili hatua zaidi za kukabiliana na uhalifu huo zichukuliwe.
Kauli hiyo aliitoa jijini hapa
wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari,ambapo
alisisitiza kutokomeza mtandao huo kabla hajasitaafu kazi katika kipindi kifupi
kijacho.
“Kwa sasa mimi ni mstaafu ila
nimekuwa nikiongezewa muda kutokana na unyeti wa kitengo hiki, hata hivyo kwa
sasa najiandaa kustaafu rasmi,ila nataka kabla sijastaafu niwe nimeufuta
mtandao huu,hata hivyo, nimejitahidi kujenga mtandao wa mawasiliano katika
nchi mbalimbali duniani unaosaidia
kufanikisha ukamataji wa wa wasafirishaji dawa za kulevya,” alisema.
Adha alisema Watanzania
wamekuwa vinara wa kuingiza na kusafirisha dawa za kulevya nchini na nje ya
nchi huku takwimu zikionesha kati ya
kesi 98 zilizoko mahakamani idadi kubwa ya washtakiwa ni Watanzania.
“Kwakweli Watanzania ndio
wanaoongoza kwenye biashara hii, wakifautiwa na raia wa Nigeria,Pakistan na
Waasia,” alisema.
Alisema kikosi chake kimepiga
hatua kubaini mbinu zinazotumiwa na wahalifu hao wakati wa usafirishaji,ikiwemo
kuwatumia akina mama wajawazito,kuweka sehemu za siri,kufunga kwenye
vifungashio vya bidhaa halali pamoja na njia mpya inayotumika kwa sasa ya
kusafirisha mali ghafi badala ya kete halisi.
Alisema wakati anaongoza kitengo
hicho mwaka 2006, alikuta kilo mbili pekee za dawa aina ya heroin
zilizokamatwa, lakini hadi kufikia Februali
2014, wamefanikiwa kukamata hadi kilo 200.5 za heroin idadi ambayo ni kubwa
kukamatwa kwa mkupuo mmoja.
Hata hivyo, alisema kazi hiyo
ni ngumu na inahitaji ujasiri wa hali ya juu kutokana na changamoto mbalimbali
ikiwemo kutishiwa kuuawa na rushwa ya
fedha.
Aliongeza kuwa ofisi yake inafuatilia
kwa makini taarifa zozote zinazotolewa na raia wema hasa baada ya kuwepo habari
kuwa kuna mtandao wa vigogo wanaojihusisha na uuzaji nausafirishaji wa dawa hizo huku akisisitiza kuwa hakuna
atakaye salimika hata kama awe na cheo gani.
“Tunathamini sana taarifa
zinazoletwa kwetu na zinatusaidia kuwanasa wahalifu, hapa nchini tumepata taarifa nyingi za
watu wakubwa ila bado tunafuatilia kwa
kina muda si mrefu utasikia tu tumekamata ila tunashangaa kwanini
hawafungwi?’’alihoji.
Akizungumzia rekodi za
ukamataji wa dawa hizo, alisema idadi kubwa ya dawa zinazokamatwa ni aina ya heroin zikifuatiwa na cocaine.
Alisema mwaka 2010 walikamata
kilo195 za heroin mkoani Tanga huku jijini Dar es Salaam, zikikamatwa kilo 179.
Alisema mwaka 2012 mkoani Lindi
walikamata kilo 211 na mwaka 2013
walikamata kilo 50 jijini Dare es Salaam.
Alioa rai kwa askari polisi
wawe waadilifu pindi wanapowakamata watuhumiwa na kuacha tamaa zisizo kuwa na
tija ili weweze kufanikiwa kutokomeza mtandao huo.
No comments:
Post a Comment