
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akizungumza na wana
Habari kuhusu ziara yake yakikazi ya siku nane Nchini Ujerumani na Oman ikiwa
ni hatua ya kukuza mashirikiano ya Wizara yake na Nchi hizo.
Mkurugenzi
Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Joseph
Kilange akimkaribisha Waziri wa wizara hiyo azungumze na wandishi wa Habari kuhusu
ziara yake yakikazi ya siku nane Nchini Ujerumani na Oman.
Na Rahma Khamis –ZJMMC.
Serikali
ya Omani imeahidi kuisaidia Sekta ya Habari Zanzibar kwa kuliwezesha Gazeti la
Zanzibar Leo kupata Mtambo wa kuchapishia Magazeti yake ili kuweza kufanya kazi
kwa ufanisi.
Aidha
nchi hiyo pia Imeahidi kuliimarisha Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kwa
kuliunganisha katika Mfumo wa Satalite ili liweze kusikiaka na kuonekana
Duniani kote.
Waziri
wa habari utalii,utamaduni , na michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk ameyasema
hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wanahabari kuhusiana na mafanikio ya
safari yake nchini Omani na Ujerumani.
Amesema
kwa muda mrefu Gazeti la Zanzibar Leo linakabiliwa na changamoto nyingi
kutokana na kuchapishwa kwa gharama kubwa nje ya Zanzibar na hivyo kama Omani
italeta Mtambo huo wa uchapishaji itasaidia sana maendeleo ya Gazeti hilo.
Kwa
upande wa ZBC Waziri Mbarour amesema Omani italeta Gari mbili za kurushia
mtangazo ya moja kwa moja na kufanya maboresho ya Studio za ZBC ili kuwa za
kisasa zaidi.
Akizungumzia
kuhusu Utalii, Waziri Mbarouk amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya
Utalii ya Omani watafanya matangazo ya pamoja ya kutangaza na kuimarisha Sekta
ya Utalii katika nchi zao.
Ameongeza
kuwa Omani itaruhusu ndege zake za Oman AIR kusafirisha watalii Wanaokuja
Zanzibar kutoka nchi tofauti ikiwa ni mwendelezo wa kuongeza Idadi ya Watalii
nchini.
Kwa
upande wa Ujerumani Waziri Mbarouk amesema nchi hiyo itaisaidia Zanzibar
kupitia Chuo cha Habari cha Zanzibar kwa kuwapatia Vifaa vya kufundishia na
kuboresha Mtaala wa Uandishi.
Aidha
amefahamisha kuwa nchi hiyo pia itatuma Walimu kutoka Ujerumani ili kuja
kufundisha masomo mbalimbali ikiwemo Lugha ya Kijerumani.
Katika
Ziara hiyo ya kikazi ya Siku nane nchini Oman na Ujerumani Waziri wa Habari
aliambatana na Viongozi waandamizi wa Wiazara yake ambapo waliweza kujadili na
kuahidiwa misaada mbalimbali kutoka nchi hizo.
No comments:
Post a Comment