Habari za Punde

Maalim Seif afungua mkutano wa Magereza Kanda ya Afrika Mashariki

Na Khamis Haji, OMKR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ni jukumu la taasisi zinazosimamia Magereza katika eneo la Afrika Mashiriki kuweka mazingira bora yatakayoweza kuhakikisha usalama na haki kwa wafungwa na watu waliomo vizuizini.

Maalim Seif amesema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Kanda unaowashirikisha wajumbe kutoka Ethiopia, Mauritius, Kenya, Uganda na Tanzania kujadili usalama magerezani, adhabu mbadala, kutokomeza dawa na kulevya pamoja na maradhi ya ukimwi uliofanyika hoteli ya Zanzibar Ocean View Migombani mjini Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais kuna kilio kikubwa miongoni mwa Mataifa tafauti kutokana na kuwepo mazingira yasiyoridhisha katika magereza hali ambayo imekuwa ni chanzo cha kuvunjwa kwa haki za wafungwa ambapo pia huchangia watu hao kupata athari za kiafya.

“Dhana yangu ni kuwa nyote mnafahamu hali duni magerezani katika nchi nyingi, hali iliyopo hata vile viwango cha chini vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa haki za wafungwa havifikiwi”, alisema Maalim Seif.

Alieleza kuwa msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza mengu inachangia kukosekan kwa huduma kama vile kupata mwangaza wa kutosha, hewa safi ambapo matokeo yake kiwango cha maradhi ya kifua kikuu na maambukizi ya ukimwi ni ya kiwango cha juu katika sehemu hizo.

Maalim Seif alisema hayo yanajitokeza licha ya kuwepo mikataba ya Kimataifa juu ya haki za watu wanaotumikia vifungo na waliopo vizuizini na kwamba mkutano huo unapaswa kuja na majibu ya namna bora kwa nchi hizo zinavyoweza kukabiliana na cvhangamoto hizo na kudumisha haki za watu hao.

“Ushauri wangu mkutano huu uzae mapendekezo ya kuwa na sera madhubuti katika kubaduilisha hali mbaya iliyopo katika magereza yetu, lakini vile vile kuja na mkakati utakaoleta ushawishi kwa serikali na taasisi zinazohusika kuweza kusimamia mabadiliko hayo”, alisema.  

Mwakilishi kutoka Shrika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya (UNODC), Jose Villa Del Castilo alisema hatua ya kubadilishana uzoefu kati ya mataifa katika masuala ya kusimamia magereza, haki za wafungwa na mbinu za kukabiliana na dawa za kulevya na msongamano wa watu magerezani ndiyo itakayoweza kusaidia kuondokana na tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.