STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 25.11.2014
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar
Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Zanzibar ina Mamlaka yake kamili na yeye
ndie Rais na kuwashangaa wanaodai Mamlaka ya Zanzibar hii leo.
Hayo aliyasema leo katika Mkutano kati yake na viongozi wa Mashina na
Maskani za CCM za Wilaya ya Kati Unguja, Mkutano uliofanyika katika viwanja vya
Hoteli ya Tamarind Uroa, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Dk. Shein aliwashangaa wanaodai Mamlaka ya Zanzibar kwani Zanzibar
inamamlaka yake kamili kwani ina nguzo zake tatu muhimu ikiwemo Mahakama Kuu ya
Zanzibar, Serikali ambayo yeye ndie Rais pamoja na Baraza la Kutunga Sheria
ambalo ni Baraza la Wawakilishi kwa hapa Zanzibar.
Alisema kuwa zipo alama mbali mbali zinazoonesha kuwa Zanzibar ina Mamlaka
yake kamili zikiwemo Bendera, Wimbo wa
Taifa, na nyenginezo na kusisitiza kuwa yoyote anaejiita msomi ni lazima
aheshimu taratibu za nchi yake, viongozi wake pamoja na wananchi kwa jumla.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mamlaka Kamili Zanzibar haiji
kwa sababu tayari Zanzibar ina Mamlaka yake kamili na kinachofanyika hivi sasa
ni upotoshwaji tu kwa wananchi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alisema kuwa Katiba iliyopendekezwa ni ya Mfumo
wa Serikali mbili hivyo aliwataka wapinzani wasiwapotoshe wananchi na
kusisitiza kuwa maelezo yake juu ya Katiba hiyo atayasema wakati wa Kampeni ukifika
ambao utakuwa ni muda wa siku 30.‘Waamuzi wa kuamua ni Wazanzibari
wote”,alisema Dk. Shein.
Ameeleza kuwa ametiwa moyo na mahudhurio makubwa aliyoyapatavyama wanataka
kuviondosha lakini mawe, tunaijua historia ya nchi yetu kabla hutajatawaliwa
hadi pale kutawaliwa na wakoloni wakiwemo Sultani wa Oman.
“Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ndipo palipoanza ukombozi na ndio
yalioikomboa Zanzibar na kufika hapa tulipofika hadi leo.... CCM haitokuwa
tayari kuwarejesha watu walioko nje ya Zanzibar, Wazanzibari wenyewe wako macho”,alisema
Dk. Shein.
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar aliwatanabahisha WanaCCM kwa wale
waliokuwa na ndoto za kuirejesha Zenj Empire ambayo ilikuwepo wakati wa ukoloni
na baada ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 Serikali ikaunda Baraza
la Manispaa liliopo hivi waondoshe ndoto zao hizo za mchana.
Dk. Shein alieleza kuwa Mabalozi wana dhamana kubwa sana na kuwataka
kuzingatia nafasi, Katiba na Utaratibu uliowekwa na chama chao na kuwataka
wawajibu wale wote wanaokibudhudhi chama hicho pamoja na na Serikali iliyopo
madarakani majibu sahihihi na yenye umakini na busara.
Aidha, Dk. Shein aliwataka viongozi hao kuwapitia wanachama wao pamoja na
wale wasiokuwa wanaCCM, na kusisitiza kuwa kiongonzi hanuni na badala yake
huwajali wanachama wote wanaomuunga
mkono na wasiomuunga mkono ili kuwavutia waingie katika chama chake.
Alisisitiza kuwa CCM inawajali sana Mabalozi wake licha ya kuwepo uchache
wa nyenzo za kufanyia kazi lakini chama hicho hakiko tayari kukiachia chama chengine
kuiongoza nchi.
Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya Muungano huku
akisisitiza kuwa kamwe Muungano huo hautovunjia na kuelezaa kuwa ataendelea
kuuulinda Muungano wa Serikali mbili kama alivyoahidi wakati wa Kampeni za
uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Dk. Shein aliwataka wananchi kutouchezea Muuungano uliopo na wasidhanie
kuwa Katiba haipo na kuwataka kuheshimu Serikali iliyopo huku akisisitiza kuwa vyama
vingi vimekuwja kuimarisha demokrasi na si kuja kukashifu serikali.
Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwataka wapinzani kutumia busara kwa serikali
iliopo madarakani na kusisitiza kuwa
Katiba ipo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo, hivyo heshima ni
lazima iwepo kwa madhumuni ya kuendeleza nchi.
Aliwataka wanaCCM kuweka mazingira mazuri ya kushinda uchaguzi kama
inavyoeleza Katiba ya CCM kuwa ni lazima kushinda uchaguzi kwani hakuna historia
wala rekodi ya CCM kushindwa uchaguzi.
Aliwahakaikishia WaCCM kuwa uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 utakuwa
uchaguzi huru na wa haki pamoja na kuwa uchaguzi wa amani na salama, na
kuwahakikishia wananchi kuwa kila mmoja atapata nafasi ya kumchagua kiongozi
anaemtaka.
Aliwataka kuwashajiiisha vijana kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la
Kudumu la Kupiga kura ili wawe na haki ya kupiga kura huku akiwataka wazee na
wazazi kuwasomesha vijana wao ili
waelewe jinsi nchi ilivyokuwa hapo kabla, ilivyo hivi sasa na itakavyokuwa hapo
baadae.
Kwa upande wa kilimo, Dk. Shein alisema
kuwa katika awamu ya saba, ruzuku, mbegu bora, dawa, pembejeo na masuala
mengine ya kilimo na kueleza kuwa Serikali imefidia kwenye kilimo na tayari
yapo matrekata mapya 20 na hivi sasa Serikali ina nia ya kuingiza matrekta 50 mapya
kwa ajili ya kuimarisha sekta hiyo.
Alisema kuwa CCM ni chama kikubwa na sio kama vyama vyengine na ndicho
kilichoikomboa Tanzania na katika ukanda mzima wa Afrika ndio miongoni mwa chama
kinachoendelea kuongoza Dola hadi leo.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akimkaribisha Dk.
Shein katika mkutano huo alieleza kuwa wanaCCM, viongozi na wananchi wote wa
wilaya kati walitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kusimamia amani na usalama wao
hasa aple palipojitokeza watu wachache kutaka kuvuruga amani.
Alieleza kuwa kumekuwa na upotoshwaji wa makusudi kutoka kwa wapinzani kuwa
Katiba iliyopendelezwa inawakandamiza Wazanzibari jambo ambalo sio la kweli na
kuaeleza kuwa Katiba hiyo ina maslahi kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.
Vuai alieleza juu ya upotoshwaji unaoenezwa hivi sasa kuwa Katiba
inayopendekezwa haimpi Mzanzibari hata Unaibu Spika wakati Ibara ya 150 kifungu
kidogo cha nne, kinaeleza kuwa Spika na
Naibu Spika watachaguliwa kutoka sehemu zote za Jamhuri ya Muungano endepao
Spika atatoka sehemu moja Naibu atatoka upande mwengine wa Jamhuri ya Muunganao
ambapo Katiba ya 1977 haikuonesha hayo.
Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar alieleza juu ya Katiba iliyopendekezwa katika Kifungu
cha Uhusiano na Uratibu wa mambo ya Muungano ambacho kinaeleza shughuli za Tume
ya Usimamia na Uratibu wa mambo ya Muungano na si kama inavyopotoshwa hivi
sasa.
"Wao waache watoe kejeli sisi tunasonga mbele katika kuimarisha miradi
ya maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi.... kamwe Muungano
hautovunjika",alisema Vuai.
Katika risala yao viongozi hao walieleza furaha yao walioyonayo kwa kuona
na kufaidika na matunda ya Dk. Shein katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa
CCM ya mwaka 2010-2015 katika maendeleo kwenye sekta mbali mbali za afya,
elimu, na miundombinu ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa kituo cha afya Ghana
na kupatiwa huduma bora katika kituo cha afya Mwera.
Aidha, walieleza kuwa kufunguliwa skuli ya Chekechea ya Cheju, skuli ya
Uzini Sekondari, Ujenzi wa barabara unaoendelea katika kijiji cha Umbuji, mradi
wa barabara ya Jumbi-Koani, Jendele-Unguja Ukuu pamoja na nyumba za makaazi ya
wananchi Mpapa na usambazaji wa maji
katika Shehia ya Dunga Bweni.
Mbali na mafanikio hayo, makubwa waliyoyaeleza viongozi hao pia, walieleza
changamoto kadhaa zinazowakabili katika uendelezaji na uimarishaji wa chama
hicho ambapo Makamo Mwenyekiti aliahidi kutekelezwa hatua kwa hatua kwa
mashirikiano ya pamoja kati yake na viongozi pamoja na wanachama wa chama
hicho.
Walimuhakikishia Dk. Shein kuwa CCM itashinda kwa kishindo katika uchaguzi
Mkuu ujao na kuahidi kupiga kura ya na kumuahidi kuwa wataendelea kushirikiana
nae katika kutekeleza na kuleta maendeleo na kumuhakikishia kuwa CCM itaendelea
kuwa imara katika Mkoa wao.
Viongozi hao pia walipata fursa ya kutoa michango, mawazo pamoja na kuuliza
masuala mbali mbali kwa Dk. Shein kwa lengo la kuimarisha na kukiendeleza chama
chao huku wakimpongeza kwa umahiri wa anaoonesha katika kuongoza Serikali ya
Umoja wa Kitaifa sambamba na utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment