Habari za Punde

SOS yakabidhi misaada kwa vikundi vya ushirika Pemba

 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla , akizungumza na Wadau wa Mpango wa kuimarisha Familia Pemba,wakati wa ufunguzi wa hafla ya kukabidhi fedha kwa vikundi vinne vya Ushirika  Kisiwani humo huko katika ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba.
 Katibu wa Kikundi cha Ushirika cha Imani ni Nguzo cha Kiuyu Mbuyuni, Time Hassan Mbayayi, akipokea Baruwa ya kukabidhiwa Fedha Tshs,13 Milioni kwa ajili ya kikundi hicho, hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba
 Ofisa Tawala wa Wilaya ya Micheweni Pemba, Ahmed Khalid , akitowa nasaha zake kwa uongozi wa SOS kwa kuvikabidhi Vikundi vitatu vya Wilaya hiyo fedha kwa ajili ya mpango wa kuimarisha Familia Pemba.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya SOS Zanzibar, Mohammed P, Bhaloo,akieleza machache juu ya mpango wa kuimarisha Familia  (FSP) Pemba kwa Wadau wa mpango huo huko kwenye Ukumbi wa Hifadhi Hotel Chake Chake.
PICHA NA BAKAR MUSSA -PEMBA. .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.