Habari za Punde

Ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tatu ya Mitandao ya Kijamii (Social Media),

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis, akiwasili katika viwanja vya Chuo cha  Zanzibar Education College (ZEC) akiwa na Mkuu wa Chuo hicho Mwalim Ussi Said Suleiman, kwa ajili ya ufunguzi wa Mafunzo ya Mitandao ya Jamii kwa Vijana yalioandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar kwa kushirikiana na  Kigamboni Community Centre KCC kutoka Dar es Salam, 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis, akiwa na Walimu wa Chuo hicho wakimshindikiza katika ukumbi wa mkutano chuoni hapo kufungua mafunzo ya siku tatu ya mitandao ya kijamii kwa Vijana Zanzibar. 
Wanafunzi wa Skuli ya VIP, ilioko katika chuoni hicho wakitowa burudani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Social Media huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanziba
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (alie simama) akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media), hawapo pichani yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar kwa kushirikiana na Kigamboni Community Centre KCC kutoka Dar es Salam, huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis

   Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi akifungua mafunzo yao ya siku tatu juu ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii  
Mhe Abdalla Mwinyi Khamis akibadilisha mawazo na Viongozi wa mafunzo hayo baada ya kuyafungua rasmin kutoa Elimu juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii, Watsap, Facebook,Blog na Twiter. 
  Mgeni rasmin Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis, akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi na washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii,(Social Media)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.