Habari za Punde

Balozi wa Harakati za "IMETOSHA!" Ndg Henry Mdimu, Apeleka Ujumbe wake Uwanja wa Taifa


Na Henry Mdimu
Tangu asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). Ila jioni hii nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la mtoto Baraka Cosmas (picha ya kwanza) ambaye usiku wa kuamkia leo amekatwa mikono yake. 
Wanasema nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea. Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa @hmgeleka. 
Kwanza nalaani kitendo hicho cha kikatili  na kuzidi kumuomba Rais wangu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi hivi. 
Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi? Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu. Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku 
tukiwa vijiweni, mmenielewa? #IMETOSHA


 Bango la harakati za "Imetosha!" likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu zete Albino. 
Wachezaji wa Yanga na Simba wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiwa wamevaa fulana maalumu za harakati za "Imetosha!"
 Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani
Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani. Marafiki hao ni mchanganyiko wa wana habari, bloggers, wasanii na wanaharakati wengine 
Rafiki wa harakati za "Imetosha!" na balozi wa Jay Millions ya VODACOM Zembwela akihamasisha akiwa na marafiki wenzie. Kulia ni mchora katuni maarufu Masoud Kipanya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa harakati hizo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.