Habari za Punde

Dk Bilal aagana na Balozi wa Japana anaemaliza muda wake

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati akimkaribisha Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 2, 2015. Balozi Okada alifika ofisini kwa Makamu kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 2, 2015, kwa ajili ya mazungumzo na kumuaga rasmi baada kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Balozi wa Japan nchini Tanzania, aliyemaliza muda wake wa kazi, Masaki Okada, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Okada alifika ofisini kwa Makamu kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.